Tuesday, November 8, 2011

DUNIANI WAWILI WAWILI Chinedu Ikedieze, (Aki) apata jiko


Taarifa zilizotolewa na Jarida la Entertainment Express la huko Nigeria linaeleza ya kwambwa super star wa Nollywood Chinedu Ikedieze aka AKI mwenye umri wa miaka 34 sasa anategemea kufunga ndoa ya kijadi na Mwanadada Nneoma siku ya jumamosi November 26 mwaka huu nyumbani kwa bi harusi Mbano katika jimbo la Imo State.
Sherehe ya harusi itafanyika Jijini lagos December 10 mwaka huu, sherehe hiyo ambayo itakuwa imepambwa na rangi nyeupe inategemea kuwavutia mamilioni ya washabiki na mastaa wa Nollywwod, Tunakutakia ndoa njema yenye mafanikio tele.

No comments:

Post a Comment