Tuesday, July 31, 2012

Riziki popote .. Kutana na Konda Rehema Juma

Mwanadada Rehema Juma ambaye ni Konda kwenye bus la Mwenge Posta
Rehema akiwa busy kurudisha chenji za abiria wake.
 Darbase leo ilifanikiwa kukutana na Konda Mwanadada mstaarabu na mchapa kazi, mke wa mtu, mama wa watoto wawili Bi Rehema Juma ambaye ni Mkazi wa Magomeni Mapipa. Ni tofauti kama inavyodhaniwa na watu wengi kuwa kazi za ukonda ni za wanaume tu lakini sio kwa dada huyu yeye alionekana kufurahia kazi yake ambayo huwa anaianza asubuhi saa 11 na kumaliza saa 2 usiku ili aendelee na majukumu yake kama mama na mke mwema. Rehema aliiambia Darbase kuwa kazi yake hiyo anaithamini sana kwani kwa siku huwa inamuuigizia kipato cha shilingi 30,000/ mpaka 40,000/.

Darbase inamtakia kila la heri Bi Rehema kwa kazi yake hiyo na pia mfungo mwema maana wakati akiongea na sisi alikuwa kwenye swaum.

Tunaomba radhi kwa ubora wa picture ila tunaahidi kukuletea full coverage ya maisha ya Rehema, challenges anazopata kwneey kazi yake na Nice photoz of course.

Did you know that Dar es Salaam is Africa's next megacity?

Dar es Salaam aerial picture
Culled from: BBC.co.uk
by Joe Boyle


Visionaries hope for a modern metropolis modelled on Singapore, but pessimists fear the emergence of another dirt-poor city of slums. Dar es Salaam is one of the world's fastest growing cities, and it has reached its tipping point.
In the dark basement of the cavernous Kariakoo market, dozens of traders gather at tiny makeshift stalls, arranging fruit and vegetables into neat piles. This part of the market has the least sought-after plots, and all of the stallholders have one thing in common: none of them was born in Dar es Salaam.
Rolens Elias arrived seven years ago from a village near Morogoro, about 150km to the west. He had been a farmer but wanted to try his luck as a trader. He now makes about 3,000 shillings ($2; £1.50) each day selling tomatoes in the farthest corner of the basement.
"It has been hard to set up a life here," he says. "I came here by myself and had to wait until I had enough money to bring my wife and family. We all live in one room, but it's a better life than in the village."
As he arranges his tomatoes, a group of his friends gather around and chip in with their own stories. They are all from Morogoro, and all came to Dar es Salaam in the hope of a better life. They all contrast the rural poverty they were born into with the lure of Dar es Salaam and its big-city opportunities.
Their stories are repeated many thousands of times across the city.

Every day new arrivals flood in, many of them setting up home in hastily erected shacks, many others sleeping on the streets. Those who cannot set up as greengrocers hawk goods, anything from baseball caps and mobile-phone chargers to bottled water and sweeping brushes.
The dramatic influx has pushed the city's population up from roughly two million two decades ago to four million today. If the government does nothing, the population will hit eight million in 20 years, according to Nimrod Mushi, a lecturer at the city's Ardhi university.
He is one of the experts commissioned by the government to produce a "master plan" to overhaul the city's infrastructure. Singapore is his role model, and he favours big projects to clear slums and build bridges, roads and out-of-town settlements.
"When we went to Singapore, we could see their satellite towns, their ring-roads, their skyscrapers and their decentralised services, and it's working very nicely there," he says.
Read more after the cut..

Monday, July 30, 2012

Tusker Project Fame Finale - Best Performance

Kwa wale ambao walifanikiwa kuangalia Finaly za Tusker Project Fame season 5 hapo jana watakubaliana na mimi kuwa the Kenyan Michael Jackson gave the best perfomance usiku wa jana ambapo wengi waliohudhuria walitumia muda mwingi kuangua kicheko mwanzo mpaka mwisho wa performance yake. MJ wa jana aliperform Thriller ambapo kidogo ilikuwa ni tofauti na the Late MJ tuliyemzowea na miondoko yake ya kujivunjavunja kwani this guy alikuwa na kazi kubwa ya kukata viuno vya upande upande ambavyo vilileta burudani ya aina yake..lol... It s too bad hatukuweza kupata Video ya tukio hili.

TANZANIA YAANZA VIBAYA OLYMPIC 2012

Bondia Kadunda wa pili kushoto mwenye Red jacket kabla ya pambano hilo. Kushoto ni kocha wake, Phares Magesa na maofisa wengine.

Bondia Kandunda baada ya pambano akiwa na some officials kwenye bus
Timu ya Tanzania inayotuwakilisha katika michuano ya Olympic ya mwaka 2012 imeanza vibaya baada ya bondia wa Tanzania Kadunda kupoteza mpambano wake jana wa kilo 69 kwa point 7-20 dhidi ya mpinzani wake Maldova's Belous. Mpambano huo ulifanyika ndani ya 'Excel Arena Boxing Venue'
Darbase tunasema kujikwaa sio kuanguka, so timu yetu iweke nguvu zaidi kwenye michezo iliyobaki ambapo mrembo Zakia anayeshikilia record ya Marathon kwa Tanzania atajaribu bahati yake kwenye kufukuza upepo wiki hii katikati.

Saturday, July 28, 2012

HONGERA MANJI...... VIJANA WAMEKUPA SHUKURANI ZAO

Mfadhili wa Yanga Yussuf Manji
Na ule mpambano kati ya Ma-don wawili wa Bongo Yussuf Manji na Bakhresa ndio umemalizika kwa bwana mdogo Manji kuibuka kidedea kwa mwaka huu wa 2012. Hiyo inatafsiriwa ni kama vijana wa Yanga kuamua kumpa shukrani zao mdhamini wao Manji kwa usajili mzuri wa mwaka huu.

NA MPIRA UMEKWISHAA... YANGA BINGWA KAGAME CUP 2012

Wachezaji wa Yanga wakiwa na furaha tele baada ya kukabidhiwa kombe lao jioni hii
 Ndani ya uwanja wa Taifa mechi kati ya Yanga FC na Azam FC imemelizika huku Ynaga ikiwa na ushindi wa magoli mawili kwa BUYU yaliyofungwa na Hamisa Kiiza dakika ya 44 na Said Bahanuzi dakika za nyongeza. kumalizika kwa mechi hiyo inamaanisha Yanga ya Dar es Salaam ndio bingwa wa Kagame Cup kwa mwaka huu. ongera Yanga kwa kundeleza  ubabe na kubakiza kombe la Kagame Jangwani.
Kiiza na Bahanuzi wote wana magoli sita ya kufunga mpaka mwisho wa kombe hili. je nani atapata kiatu cha dhahabu kati ya hao watatu wenye magoli sawa yaani 6 kila mmoja? Taddy Etikiama wa AS Vita ya Congo pia ana magoli 6.

Watani wa Jadi mpooo? semeni hongera basi hahah

SAID BAHANUZI AONGEZA GOLI LA PILI YANGA

YANGA wapata goli la pili katika dakika za majeruhi lililofungwa na SAIDI BAHANUZI

FINALI KAGAME CUP - Mpaka sasa Yanga 1 Azam 0

Hamis Kiiza akishangilia goli alilofunga dakika ya 44

Wachezaji wa Yanga wakishangilia goli lao la kwanza

Mashabiki wa Yanga wakishangilia uwanjani leo

Huu ni umati uliofurika leo uwanja wa Taifa Dar es Salaam

Mpaka sasa kipindi cha pili, Yanga wanaongoza kwa goli 1 na Azam 0. goli la kwanza la Yanga limefungwa na Hamis Kiiza dakika ya 44 kipindi cha kwanza.

Weekend photo...lol

Mhhh, how I just wish things would continue to be like this.. hahahhaha!! Tables have turned now. Je, no nani huyo muheshimiwa anayesujudiwa? mnamjua?

VIJANA WA UAMSHO DAR WAWAPA KICHAPO MACHANGU


vijana wa Kiislamu waliodai ni wa kikundi cha Jumuiya ya Uamsho Tanzania Bara walizunguka mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam na kuwashushia fimbo machangu ambao kwa sasa wametapakaa kila kona…
Vijana wa Kiislamu wenye Imani kali na wanaodai ni wa kikundi cha Jumuiya ya Uamsho Tanzania bara wiki iliyopita walileta songombingo baada ya kuwatembezea bakora machangu au dada poa kwa kudai kitendo chao cha kuendelea kujiuza kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani ni kuonyesha dharau kwa mwezi huo ambao watu wengi huwa wanauthamini na kuwa watulivu.
Safisha safisha hiyo ilianzia maeneo ya Barabara ya shekilango mpaka kituo cha mwenge ambapo kwney kila kituo cha daladala au mikusanyiko ya dada hao walisimamisha bajaji yao waliyokodi na kutembeza bakra ambapo kila dada hao walitimkia wanapopajua wao. Baada ya kumalizza zoezi hilo maeneo ya Sinza vijana hao walihamia maeneo ya Kinondoni ambapo pia biashara hiyo imeshamiri.
Hii safishasafisha campagn ilianzishwa baada ya usiku mmoja kina dada hao kumvamia muumini wa dini hiyo aliyekuwa anakwenda masjid kwa sala zake ambapo walimchezea sehemu za siri na kumuharibia udhu ambapo ilimlazimu arudi nyumbani kutia udhu upya na kurejea tena safari ya msikitini.
Photo credit: Globalpublisher.info
more pics after the cut.

OLYIMPIC, KILA LA HERI TANZANIA TIMU

Pichani ni timu yetu ya Tanzania ambayo inashiriki michuano mbalimbali ya Olympic 2012 wakionekana kupepereusha bendera yetu vizuri hapo jana katika sherehe za ufunguzi wa mashindano hayo. Tunaitikia kila la heri timu yetu hiyo japo ilete hata medali moja ya Gold.
Hey, by the way walipendeza sana na suti zao.

Friday, July 27, 2012

Olympic 2012 Opening ceremony is today – No cheap thrill

LONDON - The London 2012 opening ceremony will be a spine-tingling extravaganzathat exceeds expectations,thrilled audience members said after witnessing the final rehearsal for today's showpiece spectacular.
members on the rehesals

The Opening Ceremony is a celebration showcasing the best of the Host Nation. It also features a parade of all competing nations and the highly anticipated entrance of the Olympic Flame, which ignites the Cauldron and signals the start of the Games.
The eyes of the world will be on London for the Opening Ceremony of the London 2012 Olympic Games. The Ceremony will provide an opportunity for the world to view the artistic expression of the Artistic Director (Danny Boyle) and his team, and the culture of our Host City and the UK. There are certain elements that must feature in every Ceremony, as outlined in the International Olympic Committee (IOC) charter. The artistic performance of the Ceremony then gets underway and welcomes the world to the London 2012 Games. read more after the cut...

Swali la kizushi..


Je mpenzi wako akikusaliti utampa nafasi nyingine ya kuwa pamoja nawe?

Utajibu nini kati ya haya hapa chini;

i.                    Ndio, Kosa moja lisiwe sababu ya kuvunjika kwa muhusiano mazuri ya mapenzi kati yenu.

ii.                  LABDA, lakini mahusiano hayatokuwa kama ilivyokuwa mwanzo

iii.                Hapana, kwani ukimpa nafasi hiyo uwezekano wa yeye kurudia tena ni mkubwa. Mpotezee tu.

NI NANI KUNYAKUWA KIATU CHA DHAHABU KAGAME CUP?


Bihanuzi akiwa amembeba Hamisi Kiiza
Mchecheto wa  je ni nani kunyakuwa kiatu cha dhahabu cha Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame umezidi kupamba moto baada ya John Raphael Bocco ‘Adebayor’ wa Azam FC na Hamisi Kiiza ‘Diego’ wa Yanga kutimiza mabao matano kila mmoja, hivyo kulingana na Said Bahanuzi ‘Spider Man’ anayeshika nafasi ya pili, nyuma ya Taddy Etikiama na AS Vita ya DRC, mwenye mabao sita.
Wachezaji wote hao wanne, watakuwa na fursa ya kuongeza mabao yao Jumamosi, Bocco, Kiiza na Bahanuzi wakicheza fainali kati ya Yanga na Azam, wakati Taddy akiiongoza AS Vita katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu, dhidi ya APR ya Rwanda.    

John Bosco wa Azam Fc

Wengine waliomo kwenye kinyang’aniyo hicho ni Suleiman Ndikumana wa APR mwenye mabao mabao matatu, ambaye pia anaweza kuongeza mabao yake katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu keso.
Abdallah Juma ‘Dullah Mabao’ wa Simba SC timu yake imetolewa akiwa ana mabao mawili sawa na Leonel St Preus wa APR, Didier Kavumbagu wa Atletico, Feni Ali na Robert Ssentongo wa URA.

MSIMAMO WA MAGOLI ULIVYO:
Taddy Etikiama                 AS Vita        6
Said Bahanuzi                   Yanga SC     5
Hamisi Kiiza                     Yanga SC     5
John Bocco                       Azam FC    5
Suleiman Ndikumana       APR              3
Abdallah Juma                  Simba SC    2
Leonel St Preus                APR            2
Didier Kavumbagu           Atletico        2
Feni Ali                            URA           2
Robert Ssentongo             URA          2 

HAMIS KIIZA AIPELEKA YANGA FAINALI

Hamis Kiiza akishangilia na wachezaji wenzie wa Yanga baada ya kufunga goli la pekee jana

Mchezaji Hamis Kiiza ya Yanga mwenye asili ya Uganda jana amefanikiwa kuipeleka timu yake ya Dar Young African kwenye fainali ya kombe la Kagame kwa goli pekee alilofunga kwenye mchezo huo katika kipindi cha nyongeza. Kiiza alifunga bao hilo, kwa kichwa akiunganisha krosi ya karibu ya Haruna Niyonzima ambaye alitumia mwanya wa mabeki wa APR kuzubaa wakisikilizia maamuzi ya refa, baada ya Kiiza kuangushwa.
Yanga waliinuka na wakaanzisha shambulizi la haraka lililozaa bao hilo. Dakika tatu baada ya bao hilo, beki wa Yanga, Godfrey Taita alitolewa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja na sasa ataikosa fainali.
Katika Fainali hiyo ambayo intachezwa jumamosi katika uwanja wa Taifa Yanga watakutana na Azam Fm amabo wlaipata nafasi hiyo kwa kuitoa timu ya Simba SC kwa kipigo cha mabao 3-1 mwanzoni wiki hii. Mechi hii ambayo inatarajiwa kuwa katika mechi ngumu katika kombe hili ambapo watani wa jadi wa Yanga Simba wakiwa wanaombea watani wao wa Jadi kiwakute kile kilichowakuta wao kutoka kwa wababe hao Azam; wakati tiku ya Yanga yenyewe ikiwa na kazi mbili tofauti, moja ya kutetea kombe na ya pili kuonyesha kwamba hawako tayari kunywesha juice ya Vijoti kutoka kwa wana Azam Fc

Kikosi cha Yanga kitakachopambana Jumamosi

Kikosi cha Azamu kitakachopambana jumamosi
more pictures after the cut...

Thursday, July 26, 2012

Moyo Vs Brain


MIFUKO YA JAMII HIYO...ndani ya kikatuni

Thanks to Kipanya kwa kuliona hili kwa mbali zaidi..

Chameleon alalamikia kitendo cha kunyanganywa passport yake Tanzania

Chameleon akifanya vitu vyake kwenye tamasha la usiku wa Matumaini tar 7/7/2012 uwanja wa Taifa

Chameleon akifanya vitu vyake kwenye tamasha la usiku wa Matumaini tar 7/7/2012 uwanja wa Taifa

Lile saga la Passport kati ya C.E.O wa Global Publisher Eric Shigongo na mwanamuziki maarufu kutoka Uganda Josee Chamelion bado linaendelea baada  ya mwanamuziki huyo jana kuandika kwenye wall yake ya Facebook kulalamikia kitendo cha Mtanzania Eric Shingongo kukamatia Passport yake  kwa karibu mwezi sasa. Tukio la Shhigongo kukamata passport ya Mwanamuziki huyo lilitokea baada ya Shigongo kudai kutapeliwa $3,500 za malipo ya awali aliyodai kuyafanya kwa Meneja wa Chamelion. Kwa mujibu wa Chamelion mwenyewe ni kuwa aliyemtapeli pesa hizo sio Meneja wake bali ni tapeli  wa huko Uganda anayekwenda kwa jina la George. Mwanamuziki huyo aliandika kuomba ushauri kwa kitendo alichofanyiwa ambacho anadhani ameonewa. Angalia chini upate status ya Chameleon.



ELTON JOHN NA MUMUEWE WATARAJIA MTOTO WA PILI

The family - Sir Elton John, mumewe David na mtoto wao wa kwanza Zachary


Vituko vya mastar wa ulaya... ile couple ya mashoga wawili (Gays) Elton John 65 na David Furnish 49  ambao baada ya harusi yao walibahatika kupata mtoto wa kwanza aitwae Zachary Jackson Levon Furnish-John siku ya Chrismass mwaka 2010, wanatarajia tena kupata mtoto mwingine kutoka kwa mwanamke yuleyule waliyemtumia kupata mtoto wa kwanza (surrogate mother). Maamuzi ya kupata mtoto wa pili ni ya wao wote wawili ikiwa kila mmoja anapendelea kuwa na mtoto zaidi ya Zachary na hawapendi mtoto huyo awe mpweke.
Tunawatakia kila la heri kwa ujio wa mtoto wao wa pili na iwe familia yenye furaha na amani tele.

Wednesday, July 25, 2012

Photo of the day... hizi ndio shule zetu

Haya ndio mambo ya shule zetu za msondo ngoma...lol. jamani ukitoka hapa hata ubongo nao si unakuwa ushaganda, kitaingia kitu kweli?

William Balfour, kijana aliyeiangamiza familia ya Jennifer Hudson ahukumiwa miaka 3 jela


Kijana William Balfour pichani anaeshutumiwa kwa kosa la mauaji ya familia ya Mwanamuziki na mcheza sinema Jennifer Hudson mwaka 2008 jana tarehe 24 July alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu mfululizo jela. Aliotuhumiwa kuwauwa ni Mama mzazi wa Jennifer, Kaka yake na mpwa wake wa kiume.