Monday, September 3, 2012

TANZANIA TUNAKWENDA WAPI? FFU WAZUA BALAA TENA IRINGA

Hayati Daudi Mwangosi aliyepoteza uhai jana wakati wa vurugu za WanaChadema na FFU huko Iringa
 Jana Tasnia ya Wanahabari ilimpoteza Mwandishi Daudi Mwagosi wa Channel 10 na Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (IPC) katika vurugu zilizotokea kati ya Polisi wa kuzuiwa vurugu FFU na wanachama wa CHADEMA ambapo walikuwa wamekusanyika kwenye ofisi ya chama chao kijijini Nyololo, Mufindi tayari kwa maandamano ambayo yalikuwa yakipingwa na Serikali.
Wanachama wa Chadema wakiwa wamekusanyika nje ya ofisi ya chama chao huko Nyololo, Iringa

Polisi wakitoa amri ya watu waliokusanyika eneo hilo kutawanyika
 picha zaidi ya cut.... tahadhari picha zingine sio nzuri sana


Polisi wakiwa wamejisandaa tayari kwa lolote

Hayati Mwangosi, kulia mwenye Camera na Jacket la Khaki akiwa kazini dakika 20 kabla ya mauti yake

Polisi wa FFU wakiwa wanamshambulia Bwana Mwangosi aliyekuwa katikati hapo

FFU hapo wanaonekana wakiwa wamemaliza kazi yao

No comments:

Post a Comment