Monday, November 21, 2011

SHEREKEA MIAKA 50 YA UHURU NA FILAMU YA CPU MLIMANI CITY


WAKATI tukielekea katika kusherekea miaka 50 ya Uhuru wetu, ni wakati wako wa kuburudika na kufurahia filamu bora kabisa ya CPU, filamu hiyo iliyotengenezwa na kampuni ya Haak Neel Production kwa kushirikiana na Wegos Works zote za Jijini Dar es Salaam ni filamu ya kipekee, na ni filamu ya kwanza kushirikisha wanataaluma wengi katika tasnia ya filamu.
Tasnia ya filamu imeanza kitambo na wengi tuanaamini kuwa inakua kwa kiasi chake, ni zaidi ya miaka kumi na sita ukitoa miaka kumi ambapo filamu zimegeuka na kuwa biashara rasmi tofauti na hapo awali ambapo wengi walichukulia kama ni sehemu ya burudani tu, na si biashara ni wakati wa filamu kama Shamba Kubwa na filamu nyinginezo, japo kutoka kwa filamu hizo si mwanzo wa kuzalishwa filamu.
Filamu ya CPU ni filamu bora ambayo imeweza kushirikisha watu wenye fani na ujuzi katika fani zao, lakini kuu ni kuweza kuonyeshwa katika jumba la sinema lenye hadhi ya kimataifa wa MLIMANI CITY CINEMAX CENTURY kuanzia 25TH NOVEMBER 2011 hadi 2ND NOVEMBER 2011muda saa7:00 jioni.
Kumbuka kuwa filamu ya CPU ndio filamu ya kwanza kutengenezwa na wazawa huku ikiwa ni filamu pekee yenye sifa za kuonyeshwa katika majumba ya filamu ulimwenguni na ndio njia kwa Watayarishaji wengine kuelekea katika soko la kimataifa, baada ya miaka 50 ya Uhuru wetu filamu ya CPU inawanyanyua Watanzania kuwa ni moja kati ya watayarishaji wa filamu wakimataifa.
CPU ndio filamu pekee iliyoweza kuwakutanisha wanataaluma kutoka kila pande za sanaa, filamu hii inakuletea mtayarishaji wa muziki mahiri Afrika mashariki kutoka Mandugu Digital, Ambrose Dunga kwa kutengeneza miziki na midundo (Sound Track & Back ground music), hapa Dunga anakuonyesha uwezo wake katika kucheza na ala za filamu.
Filamu ya CPU hadithi iliyoandikwa na kijana mwenye uwezo wa hali ya juu katika uandishi Novatus N. Mgurusi na kuongozwa na Karabani, wasanii wakali vinara Sauda Simba (Maria Isabela), Nkwabi Juma (Alex Kibera), Steven Sandhu (David Kifati), Subira Wahure (Rehema Mlaki) Kulwa Kikumba, Husna Posh ‘Dotnata’, Mohamed Fungafunga ‘Jengua’ Richard Masinde, huku wasanii wengine zaidi ya mia tatu wameshiriki katika filamu hiyo ya kipelelezi huku ikibeba ujumbe kuhusu haki za watoto

No comments:

Post a Comment