Friday, August 10, 2012

AJALI ZINGINE MBILI ZA MAGARI ZATOKEA LEO ASUBUHI.


Ikiwa bado WaTanzania wanatafakari juu ya ajali ya bus la Sabena iliyotokea tar 8 na kuua watu 17, leo tena tarehe 10 ajali zingine mbili tofauti zimetokea nchini na kusababisha kupoteza maisha ya watu. Ajali moja imetokea maeneo ya mto wami na nyingine maeneo ya Lugoba.
Ajali ya Lugoba mkoani Pwani lori la mafuta limeshika moto ambapo nalo chanzo chake hakijaweza fahamika mpaka sasa.

Wananchi wa eneo hilo wamejazana katika eneo la tukio huku wengine wakijizolea mafuta yanayotoka kwenye gari ambalo lilikuwa limepamba moto wakati wote.

Ajali ya Mto Wami imehusisha magari manne ambapo kuna watu wamepoteza maisha na watu zaidi ya 15 wamejeruhiwa. Kwamujibu wa shuhuda wa ajali hiyo amesema roli la mafuta liligonga lori lingine la mi zigo na kufanya malori hayo mawili kuziba barabara. Na muda kidogo yakaja mabasi mawili ambayo yalikuwa yakotokea Nairobi ambapo la kwanza baada ya kuona njia hakuna lilikwepa kwa upande wa kulia wa barabara na kupindukia huko. Na basi lingine ambalo ni la shule huko Nairobi nalo likipofika hapo na kugundua hakuna njia lilichomokea upande wa kushoto ambalo nalo lilipinduka na kukandamiza watu wengi waliokuwa kwenye eneo hilo. Kwa mujibu wa shuhuda huyo anasema alishuhudia watu 9 wakiwa wamefariki hapohapo.
Taarifa zaidi tutawaletea baadae.
Darbase blog inatoa pole kwa wote walioathirika na ajali hii na pia inatoa wito kwa vyombo husika, madereva na abiria pia kushirikiana katika kupunguza ajali za barabarani ambazo zingine zinazuilika.

No comments:

Post a Comment