Wednesday, December 14, 2011

MWANAMAMA WA AFRIKA KUSINI ANYONGWA KWA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA

 
Kisa cha Janice Bronwyn Linden kutoka Afrika kusini ni tofauti na visa vya wasafirishaji wa madawa ya kulevya tulivyovizoea kusikia, Janice alipata mauti yake kwa kuchomwa sindano ya sumu jumatatu baada ya kukataa kukubali kosa la kukutwa na madawa ya kulevya katika uwanja wa baiyun international airport, nchini China mwaka 2008, Mahakama za china zilimuhukumu kunyongwa kwa sindano baada ya kumkuta na hatia lakini hukumu hiyo ilielezwa ingekuwa ni ya kifungo cha maisha kama Janice angekubali kosa, Janice alikataa kosa hata baada ya kupewa miaka miwili kujifikiria akiwa kifungoni, Janice alibaki na msimamo wake wa kutokuwa na hatia.

 “But, the fact that she chose not to go that route, makes one wonder whether she was really guilty or not. When one faces the possibility of death, one will say and do anything. Janice, it seemed was not prepared to go down without a fight. This case needs to be fully investigated.”A friend of the family told reporters.

Dada zake wawili waliruhusiwa kumwona na kuagana naye kabla hajapigwa sindano iliyotoa uhai wake.  RIP Janice.

No comments:

Post a Comment