Thursday, March 29, 2012

BIBI CHEKA KUTOA ZAWADI YA BASKELI SIKUKUU YA PASAKA MJINI MOROGORO

Bibi Cheka mwenye umri wa miaka 54 mkali wa kuimba bongofleva na kuchana HIP HOP
 






















MSHINDI katika shindano la kumtafuta mtoto atakaeimba wimbo wa Bi. Cheka litakalo fanyika siku ya Pasaka mkoani  Morogoro atazawadiwa zawadi ya baiskeli.

Pia katika shindano hilo mtoto atakayefanikiwa kuimba wimbo wa Naenda kusema kwa mama, wa dogo Asley, atajinyakulia Televisheni ya nchi 21.

Shindano hilo litasindikiza utambulisho wa msanii chipukizi wa muziki wa bongo fleva, Bibi Cheka, ambae ametambulisha nyumbani kwao mkoani humo.

Mkurugenzi wa kundi la Mkubwa na Wanae, Saidi Fella, aliliambia mtanzania kuwa, utambulisho huo utasindikizwa na wasanii wote wanaounda kundi lake pamoja na TMK Family.

Aliwataja wasanii hao kuwa ni Ferooz, Easy Man, Nurdin, Shilole, H Numbar, Mgogo, Dogo Muu pamoja na kundi la Khanga moja.
 
“Watoto wengine watakaoshiriki katika shindano hilo, watapewa zawadi ya mipira na madaftari,” alisema.
Fella alisema katika shoo hiyo, wasanii chipukizi wanaounda kundi la Mkubwa na Wanawe watapata nafasi ya kutambulisha nyimbo zao mpya kwa wakazi wa mji huo.
To check more of Bibi Cheka's Swaga click read more..

Hapa bibi Cheka akiwa ametoka kikazi zaidi.... bibi ni kauzu zaidi ya dagaa, ana kitu cha lace wig kichwani ... big up bibi



Hapa chini Bibi Cheka akikamua na Mh. Temba

No comments:

Post a Comment