Friday, March 2, 2012

hoja ya haja: Walioko Ughaibuni watashiriki vipi kuchangia mchakato wa katiba mpya??


Hii Hoja imenivutia sana hope wahusika watawafikiria ndugu zetu Walioko Ughaibuni.
Mimi niulize swali la msingi kwa serikali na wadau wa mabadiliko ya katiba ndani ya nchi yetu.

Kwa kuzingatia Ibara ya 21-(1)cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kama ilivyofanyiwa marekebisho toka 1977 hadi tarehe 30,Aprili 2000,kinachohusu Uhuru wa kushiriki shughuli za umma Sheria ya 1984 Na.15ib.6 Sheria ya 1994 Na.34 ya ib.4, Nanukuu,"21.-(1)  Bila  ya kuathiri masharti ya ibara ya 5, ya 39 na ya 67 ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana na masharti ya kuchagua na kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwa kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, kila raia wa Jamhuri ya  Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao, kwa kuzingatia  utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria" kifungu cha (2) kinaendelea kusomeka kuwa,nanukuu," (2)  Kila raia anayo haki na uhuru wa kushiriki kwa ukamilifu katika kufikia uamuzi juu ya mambo yanayomhusu yeye, maisha yake au yanayolihusu Taifa".

Swali: Je Serikali imeandaa utaratibu upi wa kuwashirikisha (Wabeba Boxi)  watanzania wanaoishi nje ya nchi kwa shughuli maalumu za kiserikali au binafsi na pengine kuwa na uraia wa kudumu?  wadau wa maendeleo ya Taifa wana mtizamo gani juu ya hili au nini ushauri wao kwa serikali yetu?Naomba kuwasilisha.Mdau Joachim K. Global.

No comments:

Post a Comment