Saturday, March 3, 2012

Lilian Internet wa Twanga Pepeta atua Mashujaa band..pigo lingine Twanga

BENDI ya muziki wa dansi ya Mashujaa Musica imezidi kuibomoa bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ baada ya kumyakua mnenguaji wake mahiri,Lilian Tungaraza maarufu kama ‘Intanet’.
 
Meneja wa Mashujaa Band Maximilian Luhanga alisema kwamba wameamua kuwachukua wanamuziki hao ili kuimarisha bendi yao katika idara hizo na tayari ameshasaini mkataba wa kuitumikia bendi hiyo kwa miaka miwili ambao onyesho la utambulisho linatarajiwa kufanyika jumatano ijayo katika ukumbi wa Nyumbani Lounge.
Hii ni mara ya pili kwa Bendi ya Mashujaa kuchukuwa Mwanamuziki wa Bendi ya Twanga Pepeta ambapo mapema mwaka huu ilimyakua mmoja ya waimbaji mahiri, afahamikae kwa jina la Charlz Gabriel ‘Chaz Baba’.
Lilian Internet amesema kutokana na umahiri wake atahakikisha anaitumikia vyema Bendi yake hiyo Mpya na amewataka Mashabiki wake woote kuungana nae katika  sehemu yake hiyo mpya ya kazi.

No comments:

Post a Comment