Monday, May 14, 2012

SIMBA YATOLEWA SUDAN


SIMBA SC imeshindwa kutimiza ndoto za kusonga mbele kwenye Kombe la Shirikisho la Soka Afrika, baada ya kutolewa kwa penalti 9-8 na Al Ahly Shandy ya Sudan kufuatia sare ya jumla ya tatu. Katika mchezo huo, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shandi, na kumalizika suiku huu Simba ilipoteza kwa mabao 3-0, na ndipo changamoto za mikwaju ya penalti ikatumika na  penalti za Shandy zilifungwa na Razak Yakubu, Orwa, Bashir, Saddam, Isaac Seun Malik, Faris Abdallah, Fareed Mohamed Zakaria Nasu na kipa Abdulrahman Ali. Waliofunga penalti za Simba ni Felix Sunzu, Salum Machaku, Emanuel Okwi, Shomari Kapombe, Kelvin Yondan, Victor Costa, Mwinyi Kazimoto na Amir Maftah. Eltigani alikosa kwa upoande wa Shandy wakati Mafisango na Kaseja walikosa.

No comments:

Post a Comment