Friday, August 31, 2012

Hatimae Mbuyu Twite atua Yanga kwa mbwembwe

Mbuyu Twite akionesha jezi namba 4 aliyovikwa na mashabiki wa Yanga mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege leo. Jezi hiyo ambayo imeandikwa 'RAGE' ni jina la Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage inaenokana ni kijembe kwa mahasimu hao wa Yanga ambao awali walitangaza kumsajili kwa dau la dola 30,000 kabla ya Yanga kumpandishia hadi dola 50,000.
 
Beki wa kimataifa wa Yanga Mbuyu Twite ambaye ana asili ya Congo jana aliwasili nchini Tanzania kwa mbwembwe huku akipokelewa na mashabiki wengi wa Yanga ambao walikuwa na sintofahamu ya nini hatima ya mchezaji huyo na kwa nini hakurudi bongo na wenzie walipokwenda Rwanda kwenye mechi za ikrafiki na yeye kushiriki na timu yake hiyo mpya. Hofu ilikuwa imetanda zaidi kutokana na mgogoro wa usajili wa mchezaji huyo kati ya Mahasimu wakubwa wa mpira nchini yaani Simba na Yange kila mmoja akidai kuwa amemsajili yeye kihalali.
Mashabiki wa Yanga wakiwa na furaha tele yak y kumuona mchezaji huyo waliamua kumvalisha jezi waliyoitengeza yenye namba 4 na jina la Mwenyekiti wa klabu ya Simba bwana Rage ikiwa kama ni kijembe kwa watani wao wa jadi kwani nao wakiwa chini ya Rage walidai kumsajili na kuwa angevaa jezi namba 4 . Simba walitoa dau la dola 30,000 la kumsajili mchezaji huyo na Yanga nao wakapanda dau kwa dola 50,000/.
‘Mwenye kisu kikali ndio anakula nyama, hayo ni maneno tu ya vijana wa mjini.’

Mashabiki wa Yanga wakiwa na raha tele wakati wa mapokezi JNIA

Mbuyu akihojiwa na waandishi wa habari
Picha: shukurani Dinaismail blog

No comments:

Post a Comment