Thursday, August 23, 2012

RAIS WA TFF, TENGA ACHOSHWA NA BANGI KWA WACHEZAJI


Baada soka la Tanzania kuandamwa na kashfa ya wachezaji kutumia madawa ya kulevya aina ya bangi, sasa suala hilo linakaribia kupatikana njia ya kulizuia. Raisi wa shirikisho la soka la nchini Leogdar Tenga amesema suala la matumizi ya bangi kwa wacheza soka lipo sana kwenye soka na akasisitiza kwamba ni moja vitu vikubwa vinavyochangia maendeleo ya soka Tanzania kudumaa.

Leodgar Tenga ambaye mwishoni mwa mwaka huu anamaliza muda wake wa utawala kwenye uongozi wa TFF, amesema moja ya vitu vikubwa atakavyopigania wakati akiwa bado madarakani ni kulimaliza tatizo hilo la matumizi ya marijuana na madawa mengine yasiyoruhusiwa michezoni.


"Ni kweli tatizo la wachezaji kutumia Bangi lipo sana kwenye soka letu la Tanzania. Sasa nataka kuweka wazi kwamba kuanzia msimu ujao wale watumiaji wote watakumbana na hatari kubwa ya kupata adhabu kali. Kwa sababu tunajipanga kuwa tunawafanyia vipimo kila mara wanapocheza kwa kuwashtukiza tena ili kuweza kufanikisha kulimaliza tatizo hili." - Tenga.


Katika hatua nyingine Raisi huyo wa TFF ameshangazwa na baadhi ya viongozi wa soka kuendekeza siasa za kampeni kuhusu uchaguzi ujao wa TFF na kusahau kufanya shughuli za maendeleo na kukabiliana na changamoto zinazoikabili tasnia ya mchezo wa soka nchini.

No comments:

Post a Comment