Tuesday, October 9, 2012

Kila la Heri Jessica... penye nia pana njia

Jessica akiendelea kufanya mitihani yake y aform Four akiwa wodini huku wasimamizi wakiwa pembeni yake.

Jessica akiendelea na mitihani yake kutokea wodini

MWANAFUNZI wa kidato cha nne katika Sekondari ya Alfa Germ, Morogoro, Jessica Kiliani (17), amelazimika kufanya mtihani wake wa kuhitimu elimu  hiyo akiwa wodini baada ya kufanyiwa upasuaji.

Hatua hiyo ilifikiwa baada ya mwanafunzi huyo, kuomba aruhusiwe kufanya mtihani huo licha ya kuwa  wodini akiugulia maumivu ya upasuaji aliofanyiwa na madaktari wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa zaidi ya saa mbili na kulazwa katika wodi ya wazazi namba 7B.

No comments:

Post a Comment