Haji Ramadhani ameibuka mshindi mpya wa Taji la BSS second Chance 2011, Ramadhani liwateka mashabiki na majaji waliohudhuria hafla hiyo kuanzia alipoimba wimbo wake wa Kwanza KABIBI uliopigwa na mwanamuziki mashuhuri Samba Mapangala, ustadi wake wa kuimba na kucheza haukuwashangaza wengi hasa ukitilia maanani kuwa Haji ni mwanamuziki wa bendi ya Twanga Pepeta
Mshindi wa Bongo Star Search Second Chance, Haji Ramadhan akiwa na briefcase iliyojazwa kitita cha shilingi mil.40 alizokabidhiwa kutokana na kutwaa nafasi hiyo katika shindano lililofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee. Tarehe 14/10/2011
Rodgers Lucas ambaye alishika nafasi ya pili na kuzawadiwa shilingi mil.10 , Rogers ambaye ni mahiri katika kuimba na Kupiga gitaa aliwaacha watu hoi pale alipoacha gitaa na nyimbo zake anazotunga mwenyewe na kuamua kuchanganya vionjo mbalimbali katika kuimba na kuanza kusakata Rhumba jambo ambalo liliwafanya majaji kumpatia maksi zaidi.
Mwanadada pekee ambaye alitinga fainali za shindano hilo, Bela Kombo huyu alikuwa wa nne.Kitu ambacho kilichangiwa zaidi na maamuzi yake kumualika Rapa wa Bendi ya FM academia Chitokololo kuimba naye jukwaani na kufunikwa vibaya.
Mr Flavour na Navio walitumbuiza katika fainali hizo huku wakisindikizwa na Jumanne Iddi, Mariam Mohamedi washindi waliopita, wakiwepo pia na wakali wengine Bob Junior, Peter Msechu, Joseph Anania.
Hongera Haji
ReplyDeleteHuo ndio mwanzo
Kwa nini washindi wa Bongo Star Search huwa wanapotea baada tu ya mashindano kuisha, sidhani kama hii inasaidia sanaa ya ,muziki tz kwa namna yoyote, majaji wenyewe hawajui wanafanya nini, siku moja nimemsikia majani anamponda mtu aliyeimba wimbo ambao haukuwa bongo flavor
ReplyDelete