Wednesday, October 26, 2011

Samba v/s Yanga this Saturday…..Get ready

Viingilio vya pambano la Yanga na Simba litakalofanyika Oktoba 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom vitakuwa kama ifuatavyo;
Viti vya kijani na bluu kiingilio kitakuwa sh. 5,000, viti vya rangi ya chungwa ni sh. 7,000, VIP C sh. 10,000, VIP B ni sh. 15,000 wakati VIP A itakuwa sh. 20,000.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepanga kuuza tiketi hizo siku moja kabla ya mchezo na siku yenyewe ya mechi katika maeneo ambayo yatatangazwa baadaye.
Pambano hilo linategemewa kuchezesha na Mwamuzi wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Oden Mbaga kutoka Dar es Salaam.
Waamuzi wasaidizi katika mechi hiyo ambao wote wanatambuliwa na FIFA ni Hamis Chang’walu wa Dar es Salaam ambaye atakuwa namba moja, na John Kanyenye (Mbeya) atakayekuwa namba mbili.
Mtathimini wa waamuzi (referee assessor) atakuwa Soud Abdi kutoka Arusha wakati kamishna wa mchezo huo ni Mohamed Nyange kutoka Dodoma

Ikumbukwe kuwa hivi majuzi Yanga walimrudisha Rasmi Kocha wao wa Zamani Papic mahsusi kupambana na Mnyama

Papic akiwa Kaunda



 

1 comment:

  1. na safari hii mnyama anapakatwa tu atake asitake. na naona washaanza zengwe oohh mara refarii mara kile mradi tu!! jamaa hongera pia naona mkweo ni kamishna wa mechi.. mwambie wakileta za kuleta tutawapopoa mawe vilevile.

    ReplyDelete