Monday, October 17, 2011

WANAWAKE LIVE “RE-LOUNCH”

Pichani kulia ni Mwanaharakati wa kumkomboa Mwanamke Kimapinduzi,Mtangazaji mahiri wa Kipindi cha Wanawake Live kinachorushwa na Chanel 5 a.k.a EATV,Joyce Kiria akiwa na wachangia mada mbalimbali kwenye moja ya kipindi chake alichokuwa akikiendesha hivi karibuni.Baada ya mapumziko ya ndoa na uzazi ....Libeneke linaendelea kama kawa kwa spidi ya ndege aina ya Jet,safari hii kikiwa kimesheheni ujio mpya kabisa kwako mtazamaji,Jumanne hii Joyce Kiria ndani ya EATV atakuwa na savaivas wa saratani ya matiti pamoja na madaktari kadhaa katika kuadhimisha mwezi wa saratani ya Matiti,Oktoba.Kipindi hicho kwa sasa kimekuwa kikifanya vyema na hata kupanuwa wigo wake wa kutazamwa zaidi na watu mara baada ya kufanikiwa kuunganishwa na Africa Magic Swahili Chanell ndani ya DSTV.

No comments:

Post a Comment