Friday, March 16, 2012

MABADILIKO YA KALENDA YA MASHINDANO YA UREMBO YA DUNIA YAATHIRI KALENDA ZA MASHINDANO YA MISS TANZANIA

Mkurugenzi wa Lino International Agency inayoratibu shindano la Miss tanzania Hashim Lundenga akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusiana na mabadiliko ya mashindano hayo. kulia ni Mshauri wa kamati hiyo, Dk.Ramesh Shah

Katika mkutano wa mawakala wa wanaoandaa mashindano ya urembo kutoka nchi mbalimbali duniani uliofanyika London Uingereza mwezi Novemba 2011, Tulijulishwa mabadiliko ya Kalenda ya mashindano ya urembo ya dunia. [Miss World.]

Mashindano ya urembo ya Dunia yanatarajia kufanyika mwezi August 2012 nchini China, badala ya mwezi Novemba/ Desemba kama ilivyozoeleka, ambapo washiriki kutoka nchi mbalimbali watatakiwa wawe wamefika nchini China mwezi Julai 2012.

Kutokana na hali hiyo tunalazimika kubadilisha kalenda ya mashindano yetu kama ifuatavyo:-

1.Tutatuma Mwakilishi atakayeshiriki mashindano ya urembo ya Dunia Miss World 2012.

2.Mwakilishi huyo atapatikana kwa njia ya usaili. Ambapo warembo watakaojitokeza katika usaili huo watafanyiwa mchujo na kupatikana idadi ya warembo 10 watakaopanda jukwaani katika tafrija ndogo ili kumpata Mwakilishi ambaye atabeba Bendera ya Tanzania katika Fainali za Mashindano ya urembo ya Dunia 2012. Katika mchakato huu pia itahusisha washiriki wa zamani waTanzania katika Miss World  kama bado wana vigezo hivyo, yaani inaitwa “Miss Tanzania Second Chance”

3.Tunaomba warembo wote wenye sifa na nia ya kushiriki katika mchujo wa usaili wawasiliane na ofisi zetu au Mawakala wete popote Tanzania kupata maelezo zaidi.

Mchakato wa mashindano ya Redds Miss Tanzania 2012 katika ngazi zote utaendelea kama kawaida na Mshindi wa Redds Miss Tanzania 2012 atawakilisha nchi yetu katika Fainali za Mashindano ya urembo ya Dunia mwaka 2013, akiwa na muda wa miezi [7] saba ya maandalizi.

Hii inakidhi haja na maoni ya Wadau wa fani ya urembo ya kumpa muda wa kutosha Mrembo wa Taifa kujiandaa vya kutosha kabla ya kushiriki Fainali za dunia.

No comments:

Post a Comment