Saturday, March 17, 2012

Raffel Van Exel…. Ni Yuda aliyemsaliti Whitney Houston kwa National Enquirer

Raffel Van Eel akiwa na Whitney

Raffel Van Exel pichani juu, imegundulika ndiye aliyemsaliti Whitney Houston kwa kuuza picha zake kwa Gazeti linalopenda kuandika habari za mastaa wa juu kwa kiwango kikubwa cha pesa. Picha hizo ni zile Whitney akiwa kwenye jeneza kinyume na maombi ya familia hiyo ya kutotaka picha hizo zisionekane popote. Raffel ni jamaa anayeishi kwa kupenda kuwa karibu na Celebrities wa Hollywood ambapo huwa anauza stories zao na kupata chake. Katika sherehe za kumuaga Whitney ni yeye peke yake alikuwepo hapo ambaye alikuwa sio ndugu au kuwa na shughuli yoyote iliyomfanya awepo hapo. Mama wa Whitney Houston amemuomba azipeleke pesa hizo nyingi alizopata kwenye charity ikiwa tu kama ana hofu hata kidogo kuhusu Mungu.

No comments:

Post a Comment