Friday, March 30, 2012

Taswira ya daraja la kigamboni


 Mchoro unaoonesha jinsi daraja la Kigamboni jijini Dar es salaam litavyokuwa baada ya kukamilika. Daraja hili, ambalo linajengwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) linatarajiwa kuleta chachu kubwa katika ujenzi wa mji mpya wa Dar upande wa pili wa ghuba ya Kigamboni.
China Railways Construction Engineering Group kwa ushirikiano na China Major Bridges ndio walioshinda zabuni ya kujenga daraja hili lenye urefu wa mita 680 lenye njia sita kwa gharama za TSh 214.6. Ujenzi utachukuwa miezi thelathini na sita.
Kukamilika kwa barabara hii kutaleta maendeleo na kwa kiasi kikubwa litapunguza gharama za maisha kwa wakaazi wa Kigamboni. Mbunge wa Kigamboni Dkt Faustine Ndugulile ametoa pongezi kwa Wizara ya Ujenzi kufanya shughuli zake za msingi kwa vitendo. 

Pia ameipongeza  NSSF kwa kufanikisha mchakato huu kuanza kwa kutoa asilimia 60 ya gharama hizi, akisema ushiriki wa NSSF ni mfano mzuri wa ushirikishaji wa sekta binafsi (PPP).

No comments:

Post a Comment