Master jay na mabadiliko ya biashara ya muziki Tanzania
Hivi karibuni Joakim Kimaryo a.k.a Master Jay Producer mkongwe na mmiliki
wa studio ya Mj Records alipata nafasi ya kufanya mahojiano na kituo kimoja cha
redio hapa Tanzania na katika mahojiano hayo Master Jay alitupatia historia
nzuri ya biashara ya studio za muziki zilivyoanza, Master Jay alisema kuwa hapo
kabla alikuwa anarekodi muziki bure maana wasanii walikuwa hawana uwezo na zaidi ya hapo Muziki wa bongo fleva
ulikuwa unapata nafasi finyu sana kwenye vituo vya redio mara nyingi ilikuwa
haizidi dakika tano,
Master Jay anamkumbuka Mr II,
Joseph mbilinyi kama mwanamuziki wa kwanza aliyeweza kulipa mkwanja mkubwa kwa
wakati huo pale alipoweza kulipia shilingi elfu tano( buku tano) kwa kila
nyimbo wakati aliporekodi album yake katika studio za mj records
Master Jay anasema kwa sasa kuna
utitiri wa Studio kama saloon na hakuna standard na kuna baadhi ya studio
zinatoza hata shilingi elfu arobaini kwa nyimbo moja, kitu ambacho master
anaona kinatishia uhai wa biashara ya kurekodi muziki nchini, Master Jay anaona
ni lazima kuwa na kiwango cha chini cha kutoza akitolea mfano wa kampuni za
simu na akaeleza kuwa gharama za juu
zitokane na ubora wa production au kwa lugha ya kigeni value added per
production house. Master Jay amewaasa
walioko katika biashara ya kurekodi muziki Tanzania kunzingatia ubora na kuwa
na muafaka wa kiiwango cha chini cha gharama miongoni mwao ili kufanya biashara
hiyo iwe na manufaa na endelevu. Hongera Master Jay
No comments:
Post a Comment