Monday, June 4, 2012

RAIS KIKWETE AKIWA KATIKA MAZOEZI, “WATANZANIA KITAMBI NOMA.”

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, aliye katika mapumziko mafupi jijini Arusha, akiwa katika mazoezi yake ya kila asubuhi na jioni ya kutembea kilomita 3 kabla ya kufanya mazoezi ya viungo na kuingia gym, katika kuuweka mwili wake katika hali ya ukakamavu na afya. Wakaazi wengi wa Arusha ambao wamemuona akitembea wamesisimkwa na kufurahishwa sana na hatua hiyo ya kiongozi mkuu wa nchi kuwa mstari wa mbele katika kuonesha kwa vitendo umuhimu wa kujenga afya kwa mazoezi ya kila siku, na kutaka kila mtu, si viongozi tu, kuiga mfano hai huo kwa kuanza kufanya mazoezi kila siku bila kushurutishwa  ili kulinda afya zao.



PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment