Friday, August 24, 2012

HATIMAE KALALA JUNIOR AREJEA TWANGA PEPETA

Kalala Junior jana alipokuwa na baadhi ya Wanamuziki wa Twanga Pepeta

Baada ya kukaa kimya kwa kipindi cha miezi miwili huku akiwa ametangaza kupumzika kufanya kazi na Bendi yake ya Mapacha Watatu aliyodumu nayo kama mwaka na nusu Mwanamuziki Kalala Junior hatimae jana ameweka hadharani kuwa ameamua kurudi kwenye bendi yake ya awali ya Twanga Pepeta inayomilikiwa na mwanamama Jabali Asha Baraka.
 
Katika kurudi kwake Twanga Pepeta aka nyumbani kalala ameamua kuwazawadia nyimbo mbili ambazo tayari ziitwazo  "Nyumbani ni Nyumbani" na "Ushirika ni Sawa na Koti Likikubana Livue".
Haya tena wapenzi wa Kalala Jnr na wapenzi wa Twanga mkae mkao wa kuburudika.

No comments:

Post a Comment