Thursday, August 9, 2012

OLYIMPIC 2012 - WACAMEROON 7 WAZAMIA UINGEREZA

Wacameroon walijilipua UK

Pichani juu ni Wacameroon 7 ambao jana ilibainika kutoweka kambini ambapo walikwenda kuiwakilisha nchi yao kwenye mashindano mbalimbali katika Olyimpic games za mwaka 2012. Wanamichezo hao mbao ni mabondia 5, muogeleaji 1, na msukuma kabumbu 1 yeye ni demu pekee. Mwanamke huyo  Drusille Ngako  ambaye ni golikipa kwenye timu ya mpira ya wanawake waliwakilisha nchi hiyo ndio alikuwa wa kwanza kutoroka  Baadae muogeleaji Ekane Edingue nae akafungasha virango vyake na akafuata utaritibu huo huo wa kupotea kiaina. Na mwisho kabisa wakamalizia mabondia watano ambao hawakufanikiwa  kusonga mbele kwa kisingizio cha kutafuta green pasture..
Hao wote walikuwa na Visa ya miezi 6 nchini Uingereza kwahiyo kwasasa hawana makosa yoyote ya kuishi kimakosa huko hata kama wakikamatwa, mpaka pale Visa zao zitakapokwisha.

No comments:

Post a Comment