Wednesday, October 3, 2012

Picha za ajali Mbeya jana... sad sad

Hili lori ni mojawapo y amagari matatu yalihusika kwenye ajali ya Mbarali jana ambayo imechukua maisha ya watu zaidi ya 20. kwenye lori hili kulikutwa mafuvu matatu ya vichwa ambayo inasadikiwa kuwa ni ya dereva, utingo n aabiria mmoja.
 
Hizi ni picha za ajali mbaya iliyotokea jana Katika eneo la Mbarali mbeya na watu zaidi ya ishirini wamepoteza maisha papo hapo baada ya ajali mbaya iliyo usisha lori la mafuta, daladala na pick up. Kwa heshim aya waliotangulia mbele ya haki Darbase blog haitoweza kuonyesha picha zingine za kusikitisha za vipande vya mwili wa binaadamu kama moyo, utumbo, vichwa, mbavu, miguu ambavyo vilikuwa vimezagaa eneo hilo.
Lori la mafuta likiendelea kuteketea na kuunguza eneo hilo pamoja na kinamama na watoto waliokuwa wanafua kwenye mto uliokuwepo eneo hilo.

Vipande vya watu. Vichwa miguu mikono pamoja na sehemu mbali mbali za mwili wa binaadamu vikiwa vimekusanywa kwa pamoja

Roli la mafuta likiendelea kutekea katika eneo la ajali jana

No comments:

Post a Comment