Tuesday, November 22, 2011

Mr. SUGU , ANTI VIRUS SHOW ITS ON..

Kushoto ni Msanii Fred Malaki (a.k.a- MKOLONI) na Kulia ni Mwanadada Zainab Lipangile a.k.a ZAY –B,

Waziri kivuli wa Wizara ya Habari,Vijana ,Utamaduni na Michezo na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini,Mh. Joseph Mbilinyi (a.k.a. MR. SUGU)alipata nafasi katika ukumbi wa habari maelezo kuzingumza na waandishi wa habari na wananchi kuhusu show ya Anti virus ambayo inategemewa kufanyika Dar tarehe 26 mwezi huu katika viwanja vya chuo cha ustawi wa jamii, Tamasha hilo la burudani kwa mashabiki linategemewa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali na wananchi kwa ujumla, Mbali na Tamasha la muziki ambapo wasanii mbalimbali wategemewa kutumbuiza SUGU, atatumia nafasi hiyo kuzindua rasmi kitabu chake ambacho kinaelezea historia ya maisha yake.
.Waziri kivuli wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini,Joseph Mbilinyi (a.k.a Mr. SUGU) akionyesha kitabu ambacho ameelezea maisha yake kitakachopatikana wakati wa Shoo ijulikanayo Anti Virus katika Tamasha la Burudani kwa washabiki 2011 litakalofanyika Nov. 26,2011 jijini Dar es Salaam
                          

No comments:

Post a Comment