Sunday, April 8, 2012

Wadau ... ombi maalum kwenu(a special request to you our funs)

Hellow Darbase.com funs!!! Happy Easter again!! natumai leo hii mmeifurahia vyema sikukuu ya Pasaka na familia zenu. 
wadau mnatambua kuwa hii blog yetu bado ni changa lakini kwa muda huu mfupi na kwa mapenzi yenu tumepata mafanikio makubwa sana kutokana na number of visitors kupanda kwa kiasi cha kufurahisha sana. tunawashukuru kwa hilo. bila nyinyi tusingefika hapa tulipo, mbarikiwe sana.

Hata hivyo tunapatwa na wasiwasi mmoja kuwa licha ya hatua hii nzuri tuliyofikia bila ya kuwa na feedback au maoni kutoka kwenu kidogo inakuwa inatupa wasiwasi wa kama wapi tuboreshe au wapi turekebishe au kama tumefika tulipokusudia.

Sasa kutokana na hilo tuna ombi maalumu kwenu wadau wetu, tafadhaili jisikieni huru kutupa maoni yenu ya wapi kuboresha, wapi kurekebisha na kutukosoa kwa ujumla bila ya kuwa na lugha kali isiyokuwa na lengo la kujenga.
Tunaamini nyinyi ndio mliotufikisha hapa basi na sisi tunaona kwa kuwapa heshima na shukurani ni kuwapa nafasi ya kutupa maoni yenu ili twende mbele zaidi.

Darbase.com tuko tayari kuwasikia na kufanyia kazi your input.

Bless you all.

No comments:

Post a Comment