Friday, May 18, 2012

RIP PATRICK MUTESA MAFISANGO


BIOGRAPHY
Mafisango alizaliwa Machi 30, 1980 huko Kinshasa Zaire wakati huo na ameacha mke na mtoto mmoja wa kiume, Chris Paul, mwenye umri wa miaka mitano.
Mafisango ameichezea Simba kwa msimu mmoja tu akitokea Azam ya Dar es Salaam lakini kabla ya hapo alichezea pia TP Mazembe ya DRC, APR ya Rwanda na pia aliwahi kuwa nahodha wa Amavubi kwa takribani miaka mitano.
Mwili wa Marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili tayari kwa kusafirishwa kwenda kwao Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambako atazikwa mara baada ya zoezi la kuuaga katika viwanja vya sigara kufanyika leo hii asubuhi.Ingawa alikuwa na uraia wa Rwanda na akiichezea timu ya taifa ya nchi hiyo (Amavubi), Mafisango alikuwa ni mzaliwa na raia wa DRC na uamuzi wa kuzikiwa huko ni wa familia yake.
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, Makamu wake, Geofrey Nyange Kaburu na wajumbe wa kamati ya watendaji wameeleza kusikitishwa kwao na msiba huu mkubwa kwa klabu na wamewataka wana Simba wote kuwa watulivu na kumwombea marehemu Mungu amlaze mahali pema peponi.

No comments:

Post a Comment