Mkaazi wa
kijiji cha Magomeni Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani, Khamisi Tanga (46),
ameota matiti katika hali isiyo ya kawaida ikidaiwa imesababishwa na
kutumia dawa za kupunguza makali ya Ukimwi ARV’S. Akizungumza na waandishi wa habari waliokwenda
Wilayani humo kufanya utafiti kuhusu utekelezaji wa sheria ya Ukimwi na Chama
cha Waandishi wa habari za Ukimwi (AJAT),Khamisi (Pichani) alisema alipatwa na
mkasa huo miaka mitatu iliyopita. Akisimulia namna alivyoanza
kuugua alisema awali aliona matiti yake yakiongezeka ukubwa kila kukicha lakini
hakujua kama lingeweza kuja kuwa tatizo kubwa kama lilivyo sasa.
Baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya ilimbidi kwenda kliniki anayohudhuriaga
kupata dawa na kuwaeleza manesi ambapo walimjibu kuwa imesababishwa na dawa
anazotumia na hivyo kulazimika kukatizwa dozi hiyo na kupewa aina
nyingine.
Hata hivyo Khamisi alisema kwamba
pamoja na kubadilishiwa dozi hajaona kama kuna mabadiliko yoyote aliyoyapata na
kuongeza kwamba hivi karibuni alipewa dawa nyingine ambazo kati ya hizo kuna
zile ambazo zilimsabishia matiti na tayari ameanza kupatwa na maumivu aliyokuwa
akisikiaga awali wakati matiti yalivyokuwa yanaanza kuota.
Kwa mujibu wa Khamisi ameshahangaika kupata matibabu hadi Hospitali ya
Rufaa ya Muhimbili lakini hadi leo hajapatiwa tiba stahili ya kumaliza tatizo
hilo. “Jamani Watanzania naomba wanisaidie kwa njia yoyote ile ili
niondekane na hali hii kwani inanidhoofisha sana na kunikosesha raha hasa mbele
ya wanaume wenzangu.
"Kwani
hapa navyoongea na nyie waandishi nilipimwa hadi kansa na matiti ndio kama
hivyo mnavyoyaona yanaendelea kukua na huniuma sana hasa wakati
ninapolala,”alisema kaka huyo.Pia alitumia fursa hiyo kumuomba Rais Jakaya
Kikwete kumsaidia ili arudi katika hali yake ya uanaume kwa kuwa maisha kwa
sasa kwake yamezidi kuwa magumu kwa kuwa hawezi kufanya kazi yoyote kutokana na
hali hiyo.
Mtaalam wa
magonjwa, Dk. Dina Komakoma,akielezea kuhusu sababu za kutokewa kwa hali hiyo
kwa wagonjwa wenye maambukizi ya VVU ni jambo la kawaida japo hutofautiana.
Dk. Komakoma
alisema wengine hujikuta wakinenepa au wakikonda sana na hili la Khamis sio mtu
wa kwanza kupatwa na hali hiyo na kuongeza kwamba inapotokea mgonjwa akapata
hali tofauti kama hiyo anapaswa kusitishiwa dawa
No comments:
Post a Comment