Ndugu mdau wa Sanaa,
Wadau wa Sanaa wanataalifiwa kuwa Gaba
Art Centre wataendesha warsha ya masaa mawili kuhusu Stadi za uandishi wa
miswada ya Sinema ( Script writing skills), Siku ya Jumatatu 18,June 2012, saa
4 kamili kwenye jukwaa la sanaa katika ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa
(BASATA)
Baadhi ya mambo yatakayojadiliwa ni;
1. Namna ya kuendeleza wazo hadi sinema
ya kusisimua (Idea to a good film)
2. Namna ya kufikia hisia za watazamaji
(Reaching Audience emotion)
3. Ujenzi wa Action na Dialogue nzuri.
3. Kutengeneza Wahusika (Characters)
4. Mfumo wa hadithi, Mwanzo, kati na
Hitimisho ( Ploting, beginning, middle and end)
Ni fursa nzuri kwa Wasanii kuleta
mabadiliko kwenye tasnia ya filamu kwani kumekuwa na changamoto mbalimbali katika
tasnia hii ambazo kwa njia moja au nyingine zimekuwa kikwazo katika
kufikia ufanisi unaohitajika
Mbali ya kukualika wewe binafsi,
ninakuomba uwaalike wanachama wako wote wanaoweza kunufaika na mafunzo haya.
KARIBUNI SANA
James Gayo (coordinator)
+255270006
No comments:
Post a Comment