Mratibu wa kampuni ya Bantu Film Award 2012, Stuart Kambona akizungumza na baadhi ya Wanahabari (hawapo pichani) mapema leo kwenye hotel ya Serena,jijini Dar kuhusiana na ujio mpya wa mapinduzi ya tuzo za filamu hapa nchini,kulia kwake ni baadhi ya wasanii nyota wa filamu hapa nchini.
===== ==== ====.
TUZO za kwanza kabisa za waigizaji wa filamu
zimepangwa kufanyika mwezi ujao, Mratibu wa kampuni ya Bantu Film Award, Stuart
Kambona amesema.Kambona alisema kuwa hatua ya kuanzisha tuzo hizo inatokana na
muitikio wa soko la filamu za Tanzania kwa hivi sasa tofauti na awali. Alisema
kuwa Watanzania wengi walikuwa wanapenda zaidi filamu za kigeni na kufunika
zile za hapa nyumbani.Alisema kuwa kutokana na mapinduzi
yaliyofanywa na wasanii wa fani hiyo, filamu za Tanzania kwa sasa zina soko la
hali ya juu na imtokana na tabia ya watanzania kubadili mwelekeo. Alisema kuwa
ili kuhakikisha Tanzania inafikia hatua ya Hollywood, wameamua kutoa tuzo kwa
wasanii waliofanya vizuri na kuifikisha fani hiyo katika hatua ya
sasa. BOFYA HAPA CHINI TAARIFA ZAIDI
“Tunaamini kuwa kupitia tuzo hizi, waigizaji au
wasanii wa filamu watatengeneza filamu zenye ubora wa hali ya juu ili kuweza
kutwaa tuzo na soko kwa ujumla, tunaamini tutafikia lengo letu japo tumebakisha
muda mfupi mpaka tuzo zenyewe kufanyika,” alisema Kambona.Alisema
kuwa kwa kuanzia watashindanisha filamu zote za Tanzania ambazo kwa sasa zipo
sokoni ili kutoa fursa kwa kila msanii wa fani hiyo
kushindana. Jumla ya tuzo 28 zitashindaniwa kwa mwaka huu.Baadhi ya
tuzo hizo ni Filamu Bora, Muongozaji Bora, Muigizani Bora mkuu wa Kiume,
Muigizaji Bora Mkuu wa Kike, Msaidizi Bora Mkuu msaidizi wa kike na wa kiume,
msanii chipukizi bora, filamu ya asili, Mpiga picha bora, Best Sound Track,
Best Make-Up artist, Best Costume Designer, Best
Documentary, Best Visual effect, best Film
editor, best script na Tuzo ya Heshima.Tuzo nyingine ni Outstanding
Pioneer, Best Comedian, Best Cover Design, Best producer, Best Distributor,
Best Action Movie, Best African Film outside Tanzania, Best Ligting, Best Sound
na Best Story.
Muigizaji nyota wa kike nchini, Irene Uwoya
aliwapongeza waandaaji hao kwa kuanzisha tuzo hizo ambazo alisema zitawapa
changamoto kwao kuandaa filamu za ushindani.Alishukuru kampuni ya Bantu
kwa kuanzisha tuzo hizo ambazo anaamini zitawafanya kuandaa filamu zenye ubora
wa hali ya juu."Tuzo hizi zitatufanya tufanye kazi nzuri zaidi ili
kuingia katika ushindani, natoa wito kwa waigizaji wenzangu kufanya kazi kwa
umakini ili kuleta msisimko na ushindani zaidi," alisema Uwoya.Muigizaji
Mkongwe, Jacob Steven (JB) alisema kuwa anaamini tuzo hizo zitawafikisha pale
ambao wao wamekusudia na vile vile kuibua vipaji vingine katika tasnia hiyo.JB
alisema kuwa tuzo hizo zitawafanya mashabiki wao kujua undani wa fani yao kwa
kuwajua watunzi bora, wapiga picha bora na wengineo.
No comments:
Post a Comment