Thursday, June 21, 2012

OMOTOLA 'OMOSEXY' JALADE NDANI YA BONGO


Ni onyesho maalum la familia.
MKALI wa filamu nchini Nigeria na Afrika, Omotola Jalade atazindua filamu ya Wema Sepetu Jumapili hii katika Ukumbi wa Hoteli ya Girafee Ocean View, iliyopo Mbezi Beach.Filamu hiyo iitwayo Super Star imechezwa na Wema, ikionyesha maisha ya mtu maarufu na changamoto anazozipata ikiwemo kuandikwa  mambo mbalimbali ikiwemo taarifa za vyombo vya habari.

Katika uzinduzi huo, bendi kutoka Tanzania House Of Talent (THT) watatoa burudani, kabla ya mashabiki kupata nafasi ya kupiga picha na msanii huyo. Omotola, ambaye ni mke wa rubani Kapteni Matthew Ekeinde, ambao walifunga ndoa yao angani kwenye ndege atatoa nafasi ya kupiga picha na watu kadhaa.

Katika uzinduzi huo, pamoja na burudani ya muziki, mashabiki watakaofika hapo, watapata pia fursa ya kuiona filamu ya Super Star katika viwanja hivyo vya hoteli hiyo iliyoko ufukweni. Omotola ambaye yuko kwenye ndoa kwa miaka 16 akiwa na watoto wanne, ana jumla ya albamu mbili za muziki.

Msanii huyo ambaye mwaka jana alitangaza kuachana na kucheza filamu kutokana na kuandikwa vibaya, anatarajiwa kuwa kivutio kikubwa kwenye uzinduzi huo ambao kiingilio kitakuwa Sh 30, 000 kwa wakubwa na watoto 10,000.

No comments:

Post a Comment