Friday, August 31, 2012

Earning from the Microphone - Lady Jaydee

The Bongo Flava Diva - Lady Jaydee
Lady Jaydee na mumewe Gadner siku ya ndoa yao - haya pia ni mafanikio maana asio kila mtu anapitia huku
Nyumba anayomiliki lady Jaydee
 Katika ile segment yetu ya Earning from the Mic, leo hii basi Darbase blog imeamua kurudi nyumbani na kumuangalia Diva wa Bongo Flava Lady Jaydee na mafanikio yake yaliyotokana  na muziki. gonga hiyo link hapo chini kuona picha zaidi za mafanikio ya mwanamuziki huyo

Photo of the day.. nyoka mwenye vichwa saba

Nyoka mwenye vichwa 7

Nyoka mwenye vichwa 7 akishangaliwa na watu
Duuh mie nimekuwa nikisikia tu kwenye story zetu enzi hizo za mamababu juu ya joka lenye vichwa 7, sasa sijui how true is that, ila kama inavyoonekana hapo picha watu wakimshangaa nyoka mwenye vichwa 7 anayedaiwa kaonekana Kukke Subramanya, Near Mangalore, Karnataka, India. isije ikawa photoshop tu maana siku hizi mambo ya teknolojia yamepamba moto.

Hatimae Mbuyu Twite atua Yanga kwa mbwembwe

Mbuyu Twite akionesha jezi namba 4 aliyovikwa na mashabiki wa Yanga mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege leo. Jezi hiyo ambayo imeandikwa 'RAGE' ni jina la Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage inaenokana ni kijembe kwa mahasimu hao wa Yanga ambao awali walitangaza kumsajili kwa dau la dola 30,000 kabla ya Yanga kumpandishia hadi dola 50,000.
 
Beki wa kimataifa wa Yanga Mbuyu Twite ambaye ana asili ya Congo jana aliwasili nchini Tanzania kwa mbwembwe huku akipokelewa na mashabiki wengi wa Yanga ambao walikuwa na sintofahamu ya nini hatima ya mchezaji huyo na kwa nini hakurudi bongo na wenzie walipokwenda Rwanda kwenye mechi za ikrafiki na yeye kushiriki na timu yake hiyo mpya. Hofu ilikuwa imetanda zaidi kutokana na mgogoro wa usajili wa mchezaji huyo kati ya Mahasimu wakubwa wa mpira nchini yaani Simba na Yange kila mmoja akidai kuwa amemsajili yeye kihalali.
Mashabiki wa Yanga wakiwa na furaha tele yak y kumuona mchezaji huyo waliamua kumvalisha jezi waliyoitengeza yenye namba 4 na jina la Mwenyekiti wa klabu ya Simba bwana Rage ikiwa kama ni kijembe kwa watani wao wa jadi kwani nao wakiwa chini ya Rage walidai kumsajili na kuwa angevaa jezi namba 4 . Simba walitoa dau la dola 30,000 la kumsajili mchezaji huyo na Yanga nao wakapanda dau kwa dola 50,000/.
‘Mwenye kisu kikali ndio anakula nyama, hayo ni maneno tu ya vijana wa mjini.’

Mashabiki wa Yanga wakiwa na raha tele wakati wa mapokezi JNIA

Mbuyu akihojiwa na waandishi wa habari
Picha: shukurani Dinaismail blog

BURIANI BI. HAWA NGURUME

Bi Hawa Ngurume enzi za uhai wake

Aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam na Mbalali Mkoani Iringa Bi Hawa Ngurume amefariki dunia.,
Taarifa ilizopata Darbase blog, zimesema mwanamama huyo ambaye enzi za uhai wake alikuwa kiongozi mahiri ikiwemo uwezo wa kujenga na kutetea hoja, amefariki jana asubuhi katika Hospitali ya Rufaa ya Jeshi la Wanachi wa Tanzania (JWTZ), Lugalo, Dar es Salaam.
Taarifa zimesema Mama Hawa Ngurume amefariki kutokana na ugonjwa wa Saratani, figo na vichomi.
Pia Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ametuma salamu zake za pole ambapo amesema Marehemu Hawa Ngulume, enzi za uhai wake, alikuwa kiongozi shupavu aliyesimamia maamuzi yake katika majukumu muhimu ya kitaifa kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo katika sehemu zote alizotumikia akiwa Mtumishi wa Umma, na baadaye alipopewa wadhifa wa Mkuu wa Wilaya alioutumikia katika Wilaya za Singida Mjini katika Mkoa wa Singida, Kinondoni Mkoani Dar es Salaam na mara ya mwisho katika Wilaya ya Mbarali, Mkoani Mbeya.
“Nilimfahamu Marehemu, enzi za uhai wake, kama Kiongozi Mwanamke shupavu aliyesimamia kikamilifu maamuzi yake, na hivyo kuthibitisha ukweli kwamba wanawake wakipewa fursa wanaweza”, amesema Rais Kikwete katika kuomboleza kifo chake.
Akithibitisha habari hizo, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Lugimbana amesema kuwa taarifa za mazishi zitatolewa baada ya kikao cha familia kupanga utaratibu kamili.

Tuesday, August 28, 2012

Maskini huyu Bi Harusi afa na nguo yake ya harusi wakati akifanya photo shoot

Marehemu Maria Pantazopoulos, 30 aliyefariki baada ya kuteleza mtoni akifanya photo shooting ya gauni lake la harusi
 Haya yametokea huko Canada siku ya Friday biharusi Maria ambaye alifunga ndoa mwaka huu mwezi wa sita huko huko Canada. Maria ambaye inasemekana alikuwa akilipend asana gauni lake la harusi mpaka kufikia hatua ya kuamua kufanya nalo shooting miezi miwili baada ya harusi yake inasemekana alikuwa ni mrembo, mcheshi ambaye na wakala katika Real estate business.
Gauni la harusi na mchuchumio vikionekana kuelea muda mfupi baada ya Maria kuzama mtoni

Oprah & Tyler Perry Highest paid celebrities, Forbes


Financial website Forbes.com has named the talk show queen as the highest paid celebrity for the fourth straight year.
Winfrey has failed to find major success with joint venture partner Discovery Communications on the OWN network, but her ownership in syndicated TV shows such as "Dr. Phil", "Rachael Ray", "The Dr. Oz Show" and other media products enabled her to earn an estimated $165 million between May 2011 and May 2012.
Close behind was movie director Michael Bay, whose action-packed adventure flick "Transformers: Dark of the Moon" released last year, helped him earn $160 million based on participation in ticket and toy sales and other revenue.
Another film director, Steven Spielberg, earned $130 million in the 12-month period covered by Forbes from his participation with TV shows like "Smash" and the release of the movies "The Adventures of Tintin" and "War Horse".
Jerry Bruckheimer placed fourth with $115 million from TV shows and films including "Pirates of the Caribbean: On Stranger Tides" and behind him at No. 5 was music producer Dr. Dre, who earned $110 million based mostly on the sale of part of his stake in the Beats by Dr. Dre headphone company.
Rounding out the top 10, in order, were:
Actor and producer Tyler Perry, $105 million
Radio and TV personality Howard Stern, $95 million
Author James Patterson, $94 million
Movie producer George Lucas, $90 million
Music producer and TV personality, Simon Cowell, $90 million