Monday, August 13, 2012

Hivi ndivyo Dr. Ulimboka alivyopokelewa jana

 
Kiongozi wa jumuiya ya madaktari nchini Tanzania, Dk. Steven Ulimboka, amerejea jana nyumbani akitoka Afrika Kusini katika matibabu. Dk Ulimboka amepokelewa jana na madaktari wenzake, ndugu jamaa na marafiki, alipowasili Jumapili Agosti 12, 2012, kwenye uwanja wa ndege wa kiamataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akitokea kwenye matibabu Afrika Kusini. Alisema yuko fiti na anaweza kufanya shughuli zozote atakazopewa kuanzia sasa.
Umati uliofika kumpokea

   
Kushoto ni picha baada ya kutekwa, katikati akiwasili jana, na kulia kabla ya kutekwa
Darbase blog tunamtakia Dr. Ulimboka utekelezaji mwema wa shughuli zake za kawaida na tunafurahi kumuona amerudi katika hali yake ya kawaida.

No comments:

Post a Comment