Ugandan S. Kiprotch |
Kutoka shoto Kirui (Silver), W. Kiprotchi (Bronze) na Ugandan S. Kiprotch (Gold) |
Michezo ya Olympic kwa
mwaka 2012 imemalizika jana huku majirani zetu wa Uganda na Kenya wakiwa
wanachekelea kwa ushindi walioupata katika mbio za Marathon za wanaume za kilomita 42.195 ambapo Mganda S. Kiprotich aliibuka
na medali ya Dhahabu huku Wakenya Kirui na W. Kiprotich wakipata medali ya Silver
na Bronze. Kwa kifupi matekeo yalikuwa hivi Gold: S.Kiprotich 2.08.01
Uganda ; Silver: Kirui 2.08.26 Kenya na Bronze: W.Kiprotich2.09.36 Kenya
Wakati majirani zetu wa
Afrika Mashariki wakimaliza vizuri sisi mshiriki wetu kwenye mbio hizo F. Mussa
alimaliza akiwa nafasi ya 33 na alitumia muda wa masaa 2.08.26 na Kaptain wa
Team Samson Ramadhani alimaliza akiwa wa 66 kwa kutumia masaa 2.24.52.
Mitaa ya Kampla jana
ilikuwa na shamrashamra nyingi kutokana na ushindi huo wa Gold medal ambao kwa
mara ya mwisho walizweza kupata Gold medal miaka 40 iliyopita.
Nako Kenya, Serikali ya
Kenya na wanachi wake kwa ujumla hawakufurahishwa na performance ya Timu yao
nzima iliyokwenda London kwenye Olympic mwaka huu amabpo mpak awanamaliza
wamepata Gold medal mbili tu. Kutokana na performance hiyo ilimlazima Waziri
mkuu atembelee kambi yao huko London ili kuwapa moyo na kujua tatizo ni nini.
Kwa kujitetea Viongozi wa Kenya Olympic Team wamedai kuwa kilichowagharimu ni
kosa la wao kufanya mazoezi yaliyokuwa yakishuhudiwa na Wapinzani wao na kuweza
kuibiwa techniques zao. Pia waliongeza kuwa hakukuwa na Team work kwenye timu
yao. Waziri wa Michezo wa Kenya nae akiongea jnna baada ya mashindano hayo
amesema Timu yao ya Olympic 2012 itaanza maandalizi rasmi miezi mine kuanzia
sasa ili iweze kufanya vizuri mwaka 2012.
Je, Tanzania kutokana na
hali halisi ya Team yetu na performance yetu tumejifunza nini? Tunajipanga vipi
kwa ajili ya mwaka 2016? Naipenda nchi
yangu Tanzania na ninapenda sana siku moja na sisi turudi na medali kadhaa
nyumbani. Kwahiyo muda wa maadalizi uwe na sasa na sio tusubibiri 2016!! Kila
la Heri Tanzania kwa next Olympic games.
No comments:
Post a Comment