Thursday, September 20, 2012

Photo of the day.... LOl

Viongozi wa Yanga, kushoto Mussa Katabaro na Seif Ahmad 'Magari' wakiwa taaban Uwanja wa Jamhuri jana
Hao ni viongozi wa Yanga pichani hapo jana wakiwa hawaamini kinachoondelea kweny eUwanja wa Jamuhuri Moroggoro ambapo vijana hao wa Jangwani walipigwa 3 bila. Magoli ya Mtibwa yalifungw na Dickson Daudi dk ya 11, na Hussein Javu aliyefinga magoli mawili dakika ya 43 na 86. Katika dakika ya 89 Yanga walipata penalty ambayo nayo walikosa kwani mchezaji wao Hamis Kiiza aliipaisha juu. Ama kweli siku ya kufa nyani...

Watani wanawatania walikwenda na magari ya kifahari na kurudi na Bajaji za miguu mitatu (magoli 3).. lol

Yanga kwa msimu huu kwa kweli hawakuanza vizuri ligi kwani mechi yao ya kwanza walilazimishwa suluhu ya bila kufungana na Prison.

Jana vikosi vy Ynaga na Mtibwa viliwakilishwa na hawa..
Yanga SC; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, , Mbuyu Twite/Kavumbangu, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Frank Domayo/Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Said Bahanuzi, Hamisi Kiiza na David Luhende/Stefano Mwasyika.

Mtibwa Sugar; Shaaban Hassan Kado, Malika Ndeule, Issa R Issa, Dickson Daudi, Salvatory Ntebe, Shaaban Nditi, Jamal Mnyate/Babu Seif Ally, Awadh Juma, Hussein Javu, Shaaban Kisiga ‘Malone’ na Vincent Barnabas/Ally Mohamed 'Gaucho'.


No comments:

Post a Comment