Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza majina ya Bar zitakazoshiriki shindano la Nyama Choma kwa Mikoa ya Dar na Mbeya katika hafla fupi iliyofanyika leo kwenye Hoteli ya Kebby's iliyopo Sinza Bamaga,jijini Dar.Kulia ni Jaji Mkuu Msaidizi wa Shindano hilo,Lawrance Salvi na Kushoto ni Jaji Mkuu,Douglas Sakibu |
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza majina ya baa bora zilizochaguliwa kuingia kwenye mchujo wa awali kwa mikoa ya Dar es salaam na Mbeya kwenye yale mashindano ya aina yake na ya kuvutia ya kuchoma nyama yajulikanayo kama “Safari Lager Nyama Choma 2012”.
Mashindano haya hushirikisha majiko ya baa hizo zilizochaguliwa mikoa husika ambapo utaratibu wa kuzipata ulikuwa ni kwa walaji wa nyama choma na wanywaji wa bia ya Safari kuchagua baa na jiko ambalo wanaamini kuwa linachoma nyama bomba zaidi kuliko zote.
Akizitaja baa hizo kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam meneja wa Bia ya Safari Lager Bw. Oscar Shelukindo alisema zoezi la kupata bar za mikoa ya Dar Es Salaam na Mbeya limekamilika ambapo kwa mkoa wa Dar Es Salaam bar zilizochaguliwa ni ishirini ambazo ni Huduma Bar,Rosehill garden,Kilwa Road Pub,Pentagon Pub,Texedo Garden,Gadafi Square,Angels Pub,Fyatanga Bar,Jambo Lee,Hongera Bar,Braek Point Bar,Kisuma Bar,Meeda Bar,Titanic Bar,Mangi Bar,Africenter Bar,Kisuma bar na Twiga bar wakati Mkoa wa Mbeya zimechagu ni Mbeya Carnival,City Pub,2000 Grocery,Kalembo Bar,Shaba Bar,Makasini Bar,Freepark Bar,Savoy Bar,Double J Bar na Coasini Bar.
Ambapo alisema baa hizi zimepatikana baada ya wakazi wa mikoa yote miwili kutafakari na hatimae kuamua kuzipigia kura baa hizo kulingana na umahiri wao katika uandaaji na uchomaji wa nyama choma.
Kwa sasa hatua inayofuata ni jopo la majaji kuanza kutembelea hizo bar na majiko hayo na hatimae kupata washindi watano bora kwa kila mkoa ambao ndio watapata nafasi ya kupambana katika tamasha kubwa la wazi litakalofanyika katika kila mkoa na hatimae kupatikana kwa mabingwa wa kila mkoa.
Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Mashindano hayo Jaji Douglas Sakibu aliwataka wale wamiliki na wachoma nyama wote waliofanikiwa kuingia katika hatua hii muhimu kujianda vyema ambapo zoezi la kutembelea baa hizo litaanzia jijini Mbea ambapo Jumatano ya Feb24,2012 washindi wa mkoa wa Mbeya watapata nafasi ya kushiriki kwenye semina maalumu itakayoendeshwa na majaji hao ambao ni wataalamu waliobobea katika Nyanja hizo wakiwa wote wamepata mafunzo toka katika nchi mbalimbali zilizopiga hatua kwenye uandaaji wa nyama choma.

No comments:
Post a Comment