Manuel Lemus ambaye anajulikana zaidi kama CABO SNOOP ni mwanamuziki toka nchini Angola aliyemaarufu zaidi Afrika, Si ajabu kila mwanamuziki mkali anataka kufanya naye colabo, sababu kubwa ikiwa ni Style yake ya pekee na nyimbo kali zilizoshika kila sehemu, Cabo Snoop mwenye umri wa miaka 21 alikuwepo jijini Dar Es Salaam mwezi wa kumi akihitimisha ziara yake ya Afrika mashariki mara baada ya kufanya shoo kubwa katika fainali za tusker all stars nchini Kenya katika jiji la Nairobi, yafuatayo ni mahojiano maalum na mwandishi wetu jijini Dar Es Salaam.
CABO SNOOP
Jina hili lilotokana na historia ya Nchini Angola ambako kulikuwa na Vita vya muda mrefu, Vyeo vya kijeshi kama General, Brigadier, Captain vilitawala miongoni mwa wanajeshi, CABO ni jina lililotokana na Cheo cha Captain, SNOOP imetokana na umbile lake ambalo linafanana sana na Rapper maarufu nchini marekani Snoop Dogg jina hilo alibatizwa rasmi Katika kampuni ya power house(recording label)
POWER HOUSE MUSIC
Ndio style ya muziki wake ni mchanganyiko wa wa aina ya Muziki wa Kuduro ambayo ndio muziki unapendwa zaidi nchini Angola ambao umechanganya na muziki wa Techno, RnB pamoja na Rap.
WINDEK
Ni nyimbo yake ya kwanza iliyomtambulisha, Cabo alikuwa ni Dancer na Kijana wa Kazi katika Studio za Power House, Dr Hochi Fu( Jamaa anafanana na Rick Ross ile mbaya) Ndiye mmiliki na aliyegundua Kipaji cha Cabo ambaye alimuuliza Cabo kama anaweza kuimba kwenye beat aliyoitengeneza matokeo yake yakawa ni hit windek, Huo ndio ukawa ni mwanzo wa Cabo kuwa mwanamuziki.
Windek ni jina ambalo lilianzishwa na power house records na halina maana yoyote katika lugha yoyote anayoifahamu yeye, Nyimbo hii inagusa vitu kadhaa ambavyo watu hufanya kila siku, ila ubunifu na lugha ya kuchekesha imetumika kuviwakilisha.
PRAKATATUMBA
Ni jina la kubuni ambalo lilitokana na mafanikio ya Windek, Wakina dada walianza kumfukuzia Kabo kwa kasi, Kabo na Power House wakaja na prakatatumba kuionya jamii kuwa mbali na wanaotaka wapenzi baada ya kuona wamefanikiwa kipesa na umaarufu(Gold diggers), alimalizia Cabo ambaye anamtaja 2face Idibia mwanamuziki toka Nigeria kama mwanamuziki bora zaidi anayemvutia. Kabo anasifika pia kwa style yake ya mavazi ambayo ni ya kuchanganya nguo za rangi tofauti ambayo inamtofautisha na wanamuziki wengine.
Jamaa sijui anabahati au ni mkali just dont know
ReplyDeletetumba tumba prakata tumba , jamaaa ametubamba
ReplyDelete