This is how we do it, Msanii maarufu wa Filam Tanzania Raymond kigosi, Ray the greatest naye ameripoti kubadilisha usafiri na kupata usafiri mpya kabisa ambao unafanana na mafanikio yake katika kazi za sanaa, Ray amemshukuru mungu na washabiki wote kumuwezesha kumiliki usafiri huo ambao hakupenda kueleza ametumia kiasi gani cha pesa kununua, Wasanii Filamu wanaendelea kuonyesha kuwa Sanaa hiyo inalipa bongo, Congrats bro.
Kwani Ray na Kanumba wanaigana au cause kama sijasahau kuna wakati wote walikuwa na Rav 4, now wote wamehamia magari makubwa hope wanakumbuka kujenga as well
ReplyDeleteJe hawa watu wanalipa Kodi serikalini kadri ya mapato yao wanayoingiza? Serikali inatakiwa kuangalia upya sekta ya Filam ili iweze kupata kodi kotokana na kazi za filam.
ReplyDeleteHongera Ray hayo ndio matunda ya kazi zetu. Wangapi wanaendesha magari makubwa hawalipi? Hawa wamelipa kila kitu wamepitia ofisini kwangu waache wakae wana wa wenzio wale bata. Bi up kaka. Cheers
ReplyDeleteHongera kaka Ray kwa usafiri mkubwa, ila ningependa kumshauri kaka Ray akumbuke kujiendeleza kielimu kwani nimesikia kwamba taaluma yyake ni ya ujanja ujanja. Elimu ni muhimu kwa maendeleo ya usanii na msanii mwenyewe, angalia wasanii wa Nigeria karibu asilimia tisini na nane wana digrii za kwanza. bila shule kaka Ray huwezi kuwa msanii wa kimataifa.shule itakuongezea upeo na utakubalika kimataifa. Nenda shule kaka usione aibu. good luck anyway.
ReplyDeleteHatuna tatizo na Ray na Kanumba kununua magari ya kifahari kwani hayo ni matunda ya kazi zao japokuwa bado wanaibiwa na wahuni. Of course watakiwa wamelipa kodi ya kuingiza magari yao nchini sina shaka juu ya hilo. Shaka yangu ni kama wanalipa kodi ya mapato na VAT kwa kipato kinachotokana na kazi zao za usanii. nahauri TRA wawamulike wasanii ili waweze kulipa kodi.
ReplyDelete