Thursday, January 26, 2012

BREAKING NEWS ! Mhe. GALINOMA AFARIKI DUNIA !


Aliyekua mbunge wa Kalenga,Iringa Muheshimiwa Galinoma amefariki dunia Leo mapema.
Taarifa kamili imedhibitisha kuwa mheshimiwa Galinoma amefariki
Dunia leo asubuhi mjini Iringa ndani ya gari akiwa anapelekwa hosptalini kutokea kalenga,ambako alikokuwa anaishi. Muheshimiwa Galinoma ,alikuwa mtumishi wa serikali  mstaafu aliyeshika nafasi mbali mbali katika uhai wake zikiwa Katibu mkuu idara ya ulinzi na jeshi la kujenga taifa, mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa mbuga za wanyama pori, mwenyekiti wa bodi ya mashirika ya Umma(SCOPO),Katibu wa tume ya uchunguzi wa viongozi, pia amewahi kuwa mbunge wa jimbo la Kalenga ,Iringa.
Marehemu Mhe.Bw.Galinoma alikuwa anaugua kwa mda mrefu pia aliwahi kuenda India kwa matibabu na alikua huko wiki 6 ambapo alipata nafuu kwa kiasi fulani lakini baadae alizidiwa tena.
Marehemu ameacha wajukuu na watoto ,miongoni mwa watoto wa wake ni wanamuziki Innocent na Buti Jiwe aka Henry Galinoma.
Taaritibu za mazishi zitatolewa si muda mrefu.

Mungu amlaze mahala pema peponi.

 Kwa habari zaidi za msiba wasiliana na Joseph Galinoma kwa namba hii 00255716492048 au Denis Galinoma namba hii 00255784769945

No comments:

Post a Comment