Monday, January 2, 2012

SIKU WASANII WA BONGO 50 WAKISHIRIKIANA NA AIRTEL WALIPOTOA POLE NA MSAADA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO DAR


kampuni Airtel ambayo ilikuwa imejumuka pamoja na wasanii wa Muziki nchini kwenda kutoa msaada kwa waathirika wa mafuriko waliokusanyika katika kituo cha Hananasifu kilichopo Kinondoni,jijini Dar es Salaam na Kuuaga Mwaka 2011 kwa Kutoa Huduma Kwa Jamii , Wasanii hao pamoja na Airtel wametoa msaada huo leo vikiwemo vifaa vya nyumbani zikiwemo nguo na vyakula vyote vinathamani ya Shilingi milioni 10/-
.Mtayarishaji wa Muziki (Producer) wa Bongo Flava mkongwe P Funk Majani akikabidhi sehemu ya msaada pamoja na umoja wa wasanii wa Airtel Bongo 50 kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Jordan Rugimbana maalum kwa waathirika wa mafuriko waliokusanyika katika kituo cha Hananasifu kilichopo Kinondoni
                                   
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya ‘Bongo Flava’ wa Kundi la Wanaume Halisi wakiongozwa na mkali Juma Nature na wakikabidhi sehemu ya msaada uliotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel pamoja na umoja wa wasanii wa Bongo 50 kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan Rugimbana maalum kwa waathirika wa mafuriko jijini Dar es salaam waliokusanyika katika kituo cha Hananasifu kilichopo Kinondoni,
                                                                         
Kiongozi wa Bendi ya Exta Bongo,Ally Choki akikabidhi sehemu ya msaada uliotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel pamoja na umoja wa wasanii wa Bongo 50 kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan Rugimbana maalum kwa waathirika wa mafuriko waliokusanyika katika kituo cha Hananasifu kilichopo Kinondoni

No comments:

Post a Comment