Monday, February 6, 2012
msama promotions yaomba kibali basata kuandaa tamasha la pasaka 2012
KAMPUNI ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam, imeomba rasmi kibali cha kufanya tamasha la Pasaka mwaka 2012, litakalofanyika Aprili 8, mwaka huu katika mikoa mbalimbali nchini.Akizungumza na Dira ya Mtanzania leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama, amesema tayari wamepeleka maombi BASATA ili waweze kupata kibali cha kuendesha tamasha la mwaka huu.“Tumepeleka maombi yetu ya kuandaa tamasha la Pasaka mwaka huu, tunategemea BASATA watatusikiliza na kutupatia kibali,” alisema.
Msama alisema tamasha la mwaka huu litapambwa na waimbaji wengi wa kimataifa, wakiwemo nyota wa muziki wa injili nchini.Alisema katika tamasha hilo, kamati yake itakutana kupanga sehemu litakalopofanyika tamasha hilo kwa mwaka huu.
“Miaka yote tumezoea tamasha kufanyika ukumbi wa Diamond Jubilee, lakini mwaka huu kazi ya kutafuta sehemu kubwa ya kuweza kushuhudiwa na waumini wengi wa dini ya kikristo, tumeiachia kamati, ikikamilisha tutatangaza,” alisema.
Pamoja na kusema kuwa, tamasha hilo litafanyika mikoa mbalimbali nchini, Msama alishindwa kuitaja na kusema kuwa, itatangazwa baada ya kamati yake kuichagua.Mwenyekiti huyo wa kamati ya maandalizi ya Pasaka, alisema kuwa, mgeni rasmi katika tamasha hilo atatangazwa hapo baadaye.“Suala la mgeni rasmi naomba kwa sasa mliache, linafanyiwa kazi, mambo yakikamilika, tutamweka hadharani,” alisema.
Msama alisema kuwa, mwaka jana mgeni rasmi katika tamasha hilo alikuwa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment