Wednesday, February 1, 2012

Nitatumia niliyojifunza Uswis kuendeleza fani ya mitindo-Doreen

MBUNIFU anayekuja juu kwa kasi nchini, Doreen Estazia Noni amesema kuwa atatumia aliyojifunza katika mkutano wa Uchumi Duniani kuendeleza fani yake ya ubinifu wa mavazi na maendeleo ya nchi kwa ujumla. Noni ambaye anamiliki lebo yake ya Eskado Bird alisema kuwa mkutano huo umemfungua sana katika suala la kimaendeleo na kukuza kipato kutokana na mafundisho yake. Alisema kuwa katika mkutano huo alishiriki kama mjasiliamali kupitia masuala ya mavazi, aliweza kubadilishana mawazo na kuapata uzoefu mkubwa kutoka kwa wachumi, wafanyabiashara maarufu duniani mbali ya wakuu wa nchi.  Rais Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa miongoni na tajiri maarufu duniani, Bill Gates walikuwa miongoni mwa washiriki katika mkutano huo uliofanyika nchini Uswis kuanzia Januari 25 mpaka 29.  “Najiona kama nimezaliwa upya kutokana na yale niliyojifunza na kupata uzoefu katika mkutano mkubwa wa Uchumi Duniani, nilikuwa miongoni mwa washiriki vijana 70 kutoka nchi mbali mbali 36  duniani, najisikia faraja kuwa kijana na mbunifu pekee wa Tanzania kushiriki kikamilifu katika mkutano huo,” alisema Noni. Alisema kuwa akiwa kama “Global Shapers”, aliweza kutoa mada mbalimbali ikiwa pamoja na kuzungumza na wanafunzi wa shule ijulikanyo kwa jina la Swiss Alpine katika kipengele cha ujasiliamali. Alifafanua kuwa aliweza kubadilishana mawazo na wanafunzi hao kuhusiana na nini anachokifanya ikiwa pamoja kuzungumzia lebo yake ya upande wa mavazi ya Eskado Bird hasa kampeni ya mtindo wake ujulikanao kwa jina la What's Your Freedom? (WYF?) .  Pia aliweza kuitambulisha kampuni yake ijulikanayo kwa jina la Miracle Films and Studios Limited.

No comments:

Post a Comment