Friday, April 20, 2012

January Makamba anayasema haya kwenye facebook yake...

"Asanteni sana kwa maoni yenu mengi iliyotoa katika Facebook Status yangu niliyoweka juzi kuhusu uchaguzi wa wabunge EALA: Kwa faida ya wengi, narudia maelezo yangu ya ziada niliyoweka chini ya Status ile maana nahisi wengine hawakunipata vizuri:
Napata ujasiri wa kusema yaliyojiri kwasababu sijachukua rushwa hata siku moja. Nimeumbwa na kiburi cha kukataa kununuliwa. Hata wagombea walijua hivyo Ndio maana hakuna aliyejaribu kunishawishi kwa fedha.
Taarifa zilifika TAKUKURU lakini Hakuna hatua iliyochukuliwa. Kupambana na rushwa ni suala la zaidi ya uwepo wa taasisi. Ni tabia iliyojengeka kwenye jamii yetu ya kutaka vitu au mafanikio kwa njia ya mkato. Pamoja na kuimarisha taasisi za kutafuta na kupata haki, lazima utamaduni wa haki, ukweli, maadili, na uchapakazi uanzie kwenye mioyo yetu na kwenye familia. La sivyo, hata TAKUKURU ikiwa na Ofisi kwenye kila mtaa na kila kijiji, rushwa itaendelea kushamiri.
Naambiwa wapo wahadhiri vyuo vikuu wanaomba rushwa ya ngono kuwapa gredi nzuri watoto wa kike. Rushwa ipo mahakamani, vyuoni, polisi, sekta binafsi. Tujitazame sote.

Binafsi nataraji kuanzisha mpango mahsusi ifikapo mwezi Juni kutoa mchango wangu binafsi kupambana na Kansa hii.

Asanteni sana, JM."

No comments:

Post a Comment