Kiongozi mpya wa Malawi Joyce Banda
amemtimua Waziri wake wa mashauri ya kigeni, Peter Mutharika, nduguye Rais
aliyefariki akiwa afisini.Bw.Peter Mutharika alitazamiwa kama mrithi wa
marehemu kakake katika uchaguzi wa mwaka 2014 wakati ikitazamiwa kua Rais
aliyetoweka angestaafu.
Mabadiliko haya ya baraza la
mawaziri linatokea siku chache baada ya mazishi ya aliyekua Rais.
Bibi Banda alikua ni makamu wa Rais
kuanzia mwaka 2009 lakini baadaye akakosana na Rais na kujitokeza kua mkosoaji
wake mkali. Bi Joyce Banda alilazimika kujiuzulu kutoka chama cha Democratic
Progressive mwaka 2010 alipokaidi amri ya kumkubali Peter Mutharika awe mrithi
wa rais.
Kufuatia kifo cha Bw Mutharika tareh
Aprili, kulikuepo na tetesi kua washirika wa waziri wa mashauri ya kigeni
wangejaribu kuzuia mkondo wa katiba wa kumkabidhi madaraka Bi Banda,ambaye
tangu hapo alikua ameisha unda chama chake.
www.bbcswahili.com
No comments:
Post a Comment