Mrisho Ngassa |
Hatimaye leo
mchana sakata la usajili wa mchezaji wa kimataifa wa Tanzania aliyekuwa
akiichezea klabu ya Azam msimu uliopita, kabla ya jana kuuzwa kwenda klabu ya
Simba limemalizika.
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya klabu ya Simba, leo mchana walikutana na mchezaji mwenyewe ili kuweza kukubalina juu ya mahitaji yake binafsi, baada ya jana wekundu hao wa msimbazi kumalizana na Azam.
Kwenye mkataba wake mpya na Simba, Ngassa atapewa gari aina ya Verossa, ada ya usajili millioni 30 pamoja na kupewa mshahara wa millioni 2 kwa mwezi kama alivyokuwa akilipwa kwenye klabu aliyotoka ya Azam.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari mkataba ni mwaka mmoja.
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya klabu ya Simba, leo mchana walikutana na mchezaji mwenyewe ili kuweza kukubalina juu ya mahitaji yake binafsi, baada ya jana wekundu hao wa msimbazi kumalizana na Azam.
Kwenye mkataba wake mpya na Simba, Ngassa atapewa gari aina ya Verossa, ada ya usajili millioni 30 pamoja na kupewa mshahara wa millioni 2 kwa mwezi kama alivyokuwa akilipwa kwenye klabu aliyotoka ya Azam.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari mkataba ni mwaka mmoja.
bonyeza chini kusoma zaidi
NA HUU NI UFAFANUZI
KUTOKA AZAM FC JUU YA NGASSA KUUZWA SIMBA BILA YEYE KUWA NA TAARIFA
Klabu ya Azam FC inapenda kutoa
taarifa ya ufafanuzi juu ya sakata la mchezaji Mrisho Ngasa ambalo linaonekana
kupotoshwa
1. Azam
FC ilitangaza kuwa biashara ya mchezaji Mrisho Ngasa ingefungwa siku ya
Jumatano 1/08/2012 saa saba mchana na ilivitaka vilabu vyenye interest na
mchezaji huyo kufika makao makuu ya Azam FC ofisi ndogo zilizopo kwenye kiwanda
cha unga cha Azam-Mzizima zikiwa na pesa taslimu. Bei ya mauzo iliyopangwa
ilikuwa ni Dola 50,000. Lakini katika mawasiliano ya email kwa makatibu wakuu
wa Simba na Yanga, Azam FC iliweka bayana kuwa ilikuwa tayari kushusha bei ya
mauzo na ingemuuza Ngasa kwa timu ambayo dau lake lingekuwa kubwa zaidi ya
mwenzake.
Kwa maana hiyo biashara ya mchezaji
mrisho ngasa ilifanyika kwa uwazi. Lengo la Azam FC lilikuwa ni kutoa haki kwa
kila klabu yenye uwezo wa kifedha kuweza kupata huduma ya Ngasa.
Pia tunaomba ifahamike bayana kuwa
mchezaji Mrisho Ngasa alipewa taarifa kuwa anauzwa na aliombwa asaidie
kushawishi klabu anayoitaka ifike kwetu na ofa yake. Ngasa alitamka bayana kuwa
yupo tayari kwenda klabu yoyote ambayo Azam FC itaona imekidhi mahitaji yake
kwa masharti kuwa maslahi yake ya kimkataba kati yake na Azam FC yazingatiwe.
2. Hadi
kufikia siku ya Jumatano 01/08/2012 saa saba mchana. Ni klabu ya Simba pekee
iliyojibu kwa maandishi na kuonesha nia ya kumchukua Ngasa. Yanga wao hawakuwahi
kujibu email, ingawa kwa majibu ya simu Mjumbe wao wa Kamati ya usajili Bw Sefu
Magari alitangaza kuwa Ngasa hana thamani ya zaidi ya milioni 20. Na Yanga
haikuwa tayari kuboresha ofa yake.
3. Muda
wa kufungwa kwa biashara ya kumuuza Ngasa ulipofika, ni simba pekee kupitia kwa
makamu Mwenyekiti wake Bw Geofrey Ngange na Mhasibu wake ndiyo waliofika wakiwa
na pesa taslimu shilingi milioni 25. Yanga hawakuonekana na hawakutaka kupokea
hata simu walizokuwa wakipigiwa kuulizwa kama wana interest.
4. Kikao
cha dharura cha Azam FC kilikaa na kuamua kuwa biashara ya kumuuza Ngasa
ilishindikana kutokana na kutokupatikana kwa mnunuzi mwenye dola 50,000. Kwa
maana hiyo Azam FC iliamua kumpeleka Ngasa kwa mkopo kwenye klabu iliyofika na
kuonesha nia ya kumhitaji (Simba)
5. Simba
walipewa sharti la kuhakikisha wanamlipa Ngasa mshahara wake kamili (TZsh
2,000,000) pamoja na stahiki zake nyingine zote za kimkataba
6. Sababu
za kumpeleka Ngasa kwa mkopo ni kumuepusha na adhabu ambayo klabu ya Azam FC
ingetoa kwa Ngasa kama angebaki.
7. Azam
FC inapenda kuweka wazi kuwa haijamlazimisha Ngasa kwenda Simba kama
inavyopotoshwa. Kama Ngasa anataka kuvunja mkataba wake au kama Yanga bado
wanamhitaji basi waje na dola 50,000 na Azam FC itawauzia kwani licha ya kwamba
amepelekwa kwa mkopo simba lakini Ngasa bado ni mali ya Azam FC
8. Tunaomba
kuweka msimamo wetu kuwa hatupo tayari kumlipa Ngasa na kuvunja mkataba wake na
hatuna sababu ya kufanya hivyo. Kama Ngasa hataki kwenda tunakompeleka Azam FC
inamruhusu kubakia klabuni na kutumikia adhabu.
9. Lakini
Ngasa na washauri wake waelewe kuwa akiamua kubaki Azam FC atakaa nje ya uwanja
kwa muda wote uliosalia kwenye mkataba wake, kwani Azam FC haipo tayari
kumvisha jezi mchezaji anayefanya vitendo vya utovu wa nidhamu.
10. Kwa kuwa Sakata hili
limeanza kuhusishwa na sakata la Mchezaji ramadhani Chombo. Naomba nitoe
ufafanuzi kama ifuatavyo. Redondo alipewa option tatu za kuchagua baada ya
kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu timu ilipokuwa safarini Mwanza.
a. Kupelekwa
kwa mkopo Moro United?
b. Kupatikana
kwa mnunuzi mwenye shilingi milioni 40
c. Kukubali
adhabu ya kufungiwa kwa miezi mitatu na kulipwa nusu mshahara wahati akitumikia
adhabu.
Redondo alithibitisha kuipenda Azam
FC kwa kukataa kuuzwa au kupelekwa kwa mkopo. Alikubali kutumikia adhabu yake
na ilipoisha alirudi na kuomba msamaha na sasa ni mmoja kati ya wachezaji wenye
nidhamu ya hali ya juu sana. Azam FC inajivunia kuwa na mchezaji kama Redondo
na bila kupepesa macho wala kung’ata maneno. Azam FC inamchukulia Redondo kama
mtu spesho na mwenye mapenzi ya dhati na klabu yake na inamtaka aendelee kuwa
na moyo huo.
Imetolewa na utawala.
Azam FC
No comments:
Post a Comment