Tuesday, April 3, 2012

Watanzania waanza vema katika South Africa Fashion Week

Mwanamitindo Anastazia Gura akipita mbele ya watazamaji walioshiriki katika onesho la wiki ya mavazi ya Afrika Kusini jana usiku wakati alipokuwa akionesha mavazi yaliyobuniwa na mbunifu mkubwa wa mvazi ndani na nje ya Afrika Kusini, Olive Clandle

MWANAMITINDO Anastazia Gura aliyechaguliwa na mbunifu mkubwa wa mavazi wa Afrika Kusini Olive Clandle kuonesha mavazi yake ameeleza kufurahishwa na hatua hiyo. Anastazia akihojiwa na waandishi wa habari wa hapa Afrika Kusini alisema kuwa akiwa kama mwanamitindo chipukizi kuchaguliwa kuonesha mavazi ya mbunifu huyo ni hatua kubwa kwake.

Alisema kuwa kwa kitendo cha kuchaguliwa bila hata ya kuonekana katika jukwaa ni dhahiri kuwa anavya vigezo vya kutosha na hivyo amepania kufika mbali zaidi.Anastazia alichaguliwa mara tu baada ya kuonekana akijaribisha nguo za wabunifu wa kitanzania wanaoshiriki katika onesho hilo la wiki ya mavazi.
Alifika nchini Afrika Kusini kwa lengo la kuonesha mavazi ya wabunifu watatu wa kitanzania waliochaguliwa na mwanamitindo wa kimataifa Millen Magese. Lakini hata hivyo alijikuta akichaguliwa kuonesha na mavazi ya mbunifu Olive Clande huku akiwa ndio kwanza anaingia katika tasnia ya uanamitindo huku  akiwa hajawahi hata kutembea jukwaani.

FOR MORE PICTURE  READ MORE 



Hatua hiyo imeonekana kuwashangaza waandishi wa habari wa mitindo na hata wanamitindo wengine waliopo hapa Afrika Kusini kwa kuwa mara zote mbunifu huyu hupendelea kuwatumia wanamitindo wenye majina makubwa.Akizungumzia hatua hiyo Millen alisema kuwa Anastazia na vigezo vyote vinavyotakiwa kuwa mwanamitindo na ndio maana ameweza kupatiwa nafasi hiyo kirahisi.
“Ni kwamba ili uweze kuchaguliwa inatakiwa angalau uwe na vigezo vya kimataifa ili kumwezesha mbunifu kuchagua mtu wa kumuoneshea nguo zake” alisema Millen.

Wabunifu wa mavazi wa Tanzania wakiwa wamepozi katika picha pamoja na Olive Clandle muda mfupi baada ya kumalizika kwa onesho la mbunifu huyo

Mwanamitindo mahiri Millen Magese akiwapungia mkono washabiki wake waliokuwa wakimshangilia wakati akiingiaa katika onesho hilo la mavazi ya Afrika Kusini

No comments:

Post a Comment