KOCHA MPYA STARS KIM POULSEN ATANGAZA KIKOSI KIPYA CHA TAIFA STARS.
KOCHA Mkuu wa ya soka ya taifa ya
Tanzania, Taita Stars, Kim Poulsen leo (Mei 14 mwaka huu) ametangaza kikosi cha
wachezaji 25 kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia hatua ya makundi
Kanda ya Afrika dhidi ya Ivory Coast. Akitangaza kikosi hicho ambacho kitaingia
kambini kesho kutwa (Mei 16 mwaka huu, Kim amesema uteuzi wake umezingatia
uwezo wa mchezaji uwanjani, nafasi anayocheza na ubora wake. Wachezaji
walioitwa ni makipa; Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ally (Azam) na Deogratius
Munishi (Mtibwa Sugar). Mabeki ni Nassor Masoud Cholo (Simba), Aggrey Morris
(Azam), Amir Maftah (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Simba),
Waziri Salum (Azam), Shomari Kapombe (Simba) na Juma Nyoso (Simba). Viungo ni
Mwinyi Kazimoto (Simba), Salum Abubakar (Azam), Nurdin Bakari (Yanga), Jonas
Mkude (Simba), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Edward Christopher (Simba- U20),
Mrisho Ngasa (Azam) na Frank Domayo (JKT Ruvu- U20). Washambuliaji ni Mbwana
Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo), Ramadhan Singano
(Simba-U20), Simon Msuva (Moro United- U20), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe,
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo), Haruna Moshi (Simba) na John Bocco (Azam).
Stars inayodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Kilimanjaro
itacheza mechi ya kirafiki nyumbani Mei 26 mwaka huu dhidi ya Malawi kabla
kuivaa Ivory Coast ugenini Juni 2 mwaka huu jijini Abidjan.
No comments:
Post a Comment