FFU wa Ngoma Africa band
kuvamia maonyesho makubwa International African Festival ,Tubingen
11.08.2012,Pia watapokea tuzo ya Bendi bora ya kiafrika barani ulaya Ngoma
Africa band aka FFU yenye makao yake nchini Ujerumani, Bendi hiyo maarufu
barani ulaya itatingisha tena jukwaa la onyesho ya kimataifa la International
African festival ,mjini Tubingen,Ujerumani. siku ya jumamosi 11-08 na jumapili
12-08-2012 katika uwanja wa FestPlatz, Tubingen
Habari za uhakika zinaeleza
kuwa bendi hiyo imechaguliwa kuwa bendi bora ya kiafrika barani ulaya na
kushinda tuzo la Award ya "IDA - International
Diaspora Award". tuzo hilo
litakabidhiwa kwa kiongozi wa bendi hiyo mwanamuziki mahiri Kamanda Ras Makunja
usiku wa Jumapili
2012,Kikosi kazi cha Ngoma Africa band kimepigiwa kura nyingi na
washabiki,pamoja na tahasisi mbali mbali kwa kutajwa kuwa ndio bendi pekee ya
kiafrika barani ulaya iliyoweza kutumia muziki wake kama daraja na kufanikiwa
kuziteka nyoyo za washabiki na kuwaunganisha washabiki wa mataifa mbali
mbali duniani. Pia kikosi kazi hiko kimetajwa mara nyingi kuwa kimediliki
kujitoa muanga kwa kupiga muziki mpaka kwenye nchi zenye usalama mdogo na
mazingira ya kivita !kwa ujasili huu Ngoma Africa band inavuna inachopanda
Ngoma Africa band imetajwa
kuwa muziki wake umefanikiwa kuzoa mamilioni ya washabiki na kuchangia kwa
kiasi kikubwa kutukomeza fikira za kiubaguzi wa rangi zilizomo kwa baadhi ya
wazungu barani ulaya.
Ngoma Africa band
inasemekana kuwa na washabiki au wafuasi milioni 50 dunia nzima,na washabiki
wengine milioni 11 wanapitia tovuti ya bendi hiyo at http://www.ngoma-africa.com
au www.ngoma-africa.com miongoni mwa wapenzi hao ni
wapo wanawake na wanaume , watoto ,vijana na wazee wenye rika na mataifa mbali
mbali, bila kujali itikadi za dini na matabaka ya maisha yao,wote wapo chini ya
kivuli cha mzuka wa muziki wa Ngoma Africa Band aka FFU inayoongozwa na kamanda
Ras Makunja aliyepindia akili kazi yake
No comments:
Post a Comment