Friday, September 7, 2012

Miili ya watu waliofukiwa n akifusi yapatikana

Miili ya wachimbaji madini waliokuwa mawefukiwa na kifusi
Hatimae miili ya watu wote 7 waliokuwa wamefukiwa na kifusi katika Machimbo ya Madini ya Kata ya Nandauangwa mkoani Lindi imepatikana jana. Akielezea kw aundani Diwani wa kata hiyo Bwn. Andrew Chikongwe amesema zoezi hilo limechukua muda wa siku mbili kufanikiwa kutokan ana vifaa duni walivyokuwa navyo. Amewataja walifariki katika tukio hilo ni Marehemu Nyang'awa Mkelecha(Mkazi wa Musoma), Mohamed Omari Fondogoro (Morogoro), Bakari Liganga (Chunyu), Rajabu aka Roger (Musoma), Uwesu Bakari Abeid (Rondo), Chakode (DSM) na Rashid Ally aka BADE (Mtwara). Mungu azilaze mahali pema roho za marehemu.
shughuli ya uokoaji ikiendelea

No comments:

Post a Comment