Friday, September 7, 2012

WAMAMA WA KIKUNDI CHA ‘SITAKI MUME’ WAMPA KICHAPO MBAKAJI

Dizaini za 'Wamama Sitaki Mume'

Kikundi cha wanawake wababe wa Kenya eneo la Kibera maarufu kama ‘Wamama Sitaki Mume’juzi walitoa kali baada ya kumpa kipigo mwanaume anayekwenda kwa jina la James Nyabuto  ambaye walimshutumu kumbaka mtoto wa kike wa miaka sita(6). Wamama hao waliamua kujichukulia hatua mkononi dhidi ya mtuhumiwa huyo baada ya kesi yake kuahirishwa na Mahakama ambapo walisema hawana imani na mahakama  maana kesi ya mbakaji huyo imechukuwa muda mrefu sana kuamuliwa na Mtuhumiwa yuko nje kwa dhamana tangu January 7 mwaka huu alipotenda kosa hilo. Mtuhumiwa huyo aliokolewa na Polisi waliokuwa karibu na eneo na Mahakama na huku Maofisa wengine wakiwapoza wamam hao na kuwaambia wawe wavumilivu tu kwani haki itatendeka.

No comments:

Post a Comment